Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza kumbukumbu ya kifo cha Ummul Banina (a.s)…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba ya kuomboleza kifo cha Ummul Banina Fatuma bint Hizaam (a.s) mama wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na ndugu zake walio uawa Karbala pamoja na bwana wa Mashahidi Hussein (a.s), kifo chake kinasadifu Ijumaa ya kesho mwezi kumi ya tatu Jamadal-Thani.

Ratiba ya maombolezo itadumu siku tatu kuanzia siku ya Alkhamisi (12 Jamadal-Thani), kutakua na kumbukumbu maalum ya bibi huyu ambaye ni miongoni mwa wanawake watukufu, wanao fahamu haki za Ahlulbait (a.s), iliye kua na ikhlasi kwao, na aliwapenda sana, na yeye alikua na nafsi kubwa kwao, hivyo kutakua na ratiba maalum ya ki-ibada kwa kushirikiana na watumishi wa haram ya Imamu Hussein (a.s), aina hii ya maombolezo imezoweleka kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya, kutakua na kaswida na mashairi ya kuomboleza.

Ratiba hii inahusisha pia kuupamba ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mapambo meusi, na vitambaa vyenye ujume wa kuomboleza, pamoja na kufanya majlisi za kuomboleza ambazo zitaendelea hadi siku ya Juma Pili na watashiriki makhatibu mbalimbali, pamoja na majlisi ya matam itakayo ongozwa na muimbaji mashuhuri Basim Karbalai, hali kadhalika kutakua na vikao vya kuomboleza vitakavyo fanyika katika ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa upande mwingine, vitengo vya ulinzi na vya utumishi vimetangaza kua vimejipanga kupokea waombolezaji na mawakibu za kuomboleza zitakazo kuja kutoa pole kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na msiba huu.

Kumbuka kua Ummul Banina (a.s) baada ya kumtumikia bwana wa mawasii na watoto wake maimamu wawili Hassan na Hussein (Hassanain) na Aqilah bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), umri wake mtukufu aliutumia kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu, na aliishi na huzuni kipindi kirefu kutokana na kuwakosa mawalii wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na matukio ya kutisha aliyo shuhudia, kuanzia kuuawa kwa Imamu Ali bun Abu Twalib kwa kupigwa panga katika mihrabu yake, na kifo cha mwanae Imamu Hassan (a.s), na kuuawa kwa watoto wake wanne ndani ya saa moja, waliokua wakilinda heshima ya mpenzi wa Mwenyezi Mungu na mjukuu wa mtume wake Imamu Hussein (a.s), baada ya kushuhudia yoto hayo alifariki mwezi kumi na tatu Jamadal-Thani mwaka wa 64 hijiriyya, akaenda katika rehma za Mola wake mtukufu na akazikwa katika makaburi ya Baqii karibu na kaburi la Ibrahim, Zainabu, Ummu Kulthum, Abdallah, Qassim na wengineo miongoni mwa maswahaba na mashahidi, kaburi lake lilibomolewa na manawaasib pamoja na makaburi ya maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Amani iwe juu ya mwanamke mtukufu na mtakasifu, mtekelezaji mwenye ikhlasi, aliye fata nyayo za mbora wa wanawake wa ulimwenguni Fatuma Zaharaa (a.s) kisheria na kimwenendo, pongezi kubwa ziwe juu yake na juu ya kila atakaye fuata mwenendo wao miongoni mwa wanawake wema.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: