Miongoni mwa ratiba za kongamano la Ruhu Nubuwwah: Ni ufunguzi wa maonyesho ya kazi za kiufundi…

Maoni katika picha
Kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah awamu ya pili linalo simamiwa na idara ya shule za Alkafeel za wasichana za Atabatu Abbasiyya tukufu kuanzia siku ya tarehe (8-9-10 Machi 2018m) sawa na (19-20-21 Jamadal-Thani 1439h) chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatuma (a.s) ni chemchem ya utume na tunda la peponi) limehusisha vipengele tofauti, miongoni mwa vipengele vyake ni maonyesho ya kazi za kiufundi, (Picha nzuri, Kazi nzuri, Hati nzuri, Bango zuri na picha nzuri ya mnato (photography)), vitu vinavyo shiriki katika maonyesho haya vimechaguliwa kutoka katika shindano la kongamano lililo fanywa na kupata washiriki wengi kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Maonyesho hayo yamefunguliwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, yana husisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na: Mabango ya kiufundi, kazi za mikono, picha za mnato pamoja na mabango ya hati.

Msimamizi mkuu wa maonyesho haya Israa Hamidi kutoka katika shule za wasichana za Alkafeel umeuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho haya ni matokeo ya shindano lililo tangazwa muda mrefu, na tukapata vitu vingi vya kiufundi vilivyo shiriki katika shindano hilo, vitu hivyo vikawasilishwa katika kamati maalumu kwa ajili ya kuvichuja na kuchagua washindi, pamoja na kubaini vitu vitakavyo shiriki katika maonyesho, uzuri wa maonyesho haya ni kua na vitu vingi vya aina tofauti, hii inaonyesha kuongezeka kwa ufundi katika jamii ya wanawake”.

Akaongeza kusema kua: “Kamati iliweka masharti ya kushiriki, miongoni mwa masharti hayo ni: Kuzingatia mazingira halisi na kuheshimu maelekezo ya kamati ya usimamizi pamoja na kutengeneza kitu kinacho endana na anuani ya kongamano, kamati iliandaa zawadi kwa washindi wa kila kikundi miongoni mwa vikundi vya mashindano, pamoja na kutoa vyeti vya ushiriki kwa washiriki wote hadi wale ambao vitu vyao havikufaulu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: