Kamati ya maandalizi ya kongamano la Ruhu Nubuwwah: Tumeishi na Zaharaa (a.s) katika siku ambazo zilikua kama tupo peponi kwa muda…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Ruhu Nubuwwah la mwaka wa pili kupitia ujumbe ulio wasilishwa na rais wa kamati hiyo, Ustadhat Bushra Jabbaar katika kufunga moja ya program za kongamano hilo amebainisha kua: “Ardhi ya Karbala ni ardhi ya kujitolea na fidia, siku tatu zilizo pita imepata utukufu wa kua mwenyezi wa kongamano la Ruhu Nubuwwah la pili baada ya kupita mwaka tangu kufanyika kongamano la kwanza, limepata mafanikio ambayo tunataraji wasimamizi wake wapate thawabu mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu na wapate radhi za mbora wa wanawake Batuli Mardhiyya, Mwenyezi Mungu ametaka kutuwafikisha kufanya tena kongamano hili katika ardhi hii tukufu iliyo takasika kwa utukufu wa bwana wa mashahidi na mawakibu (misafara) ya shahada katika zama zote, hakika tumeishi na Zaharaa (a.s) katika siku ambazo zilikua kama tupo peponi kwa muda.

Siku ya kwanza: Ilikua ya kutoa pongezi kwa watu walio jitolea zaidi yetu, walijitolea shahada wao na familia zao, watu ambao wameleta ushindi kwa damu zao na kwa machozi ya familia zao ushindi unaendelea dhidi ya nguvu za magaidi walio potea, wamelinda maeneo matukufu na wamehifadhi heshima na utukufu, tunacho kifanya hapa ni tunda miongoni mwa matunda ya kujitolea kwao. Kisha tuliangalia maonyesho ya kazi za kiufundi, hati za kiarabu, vitu vya kutengeneza kwa mikono mitukufu ya mabinti wa Alkafeel, kwa ajili ya kuwafanya kua walimu madhubuti, waelewa wa kujitolea kwa bibi Fatuma, na kuhakikisha haki na watu wake wanashinda, na kukataa batili na watu wake, na kuto kwenda kinyume na mafundisho ya Mwenyezi Mungu yaliyo fundishwa na mtukufu mtume na waja wema katika wanae, lilipo zama jua la siku ya kwanza zikasikika sauti za utajo na mnung’uniko wa kisomo cha kitabu kitukufu cha Qur’an kikisindikiza miale ya jua mbinguni kwa upole na unyenyekevu, wale ambao anapo tajwa Mwenyezi Mungu nyoyo zao hutetemeka.

Siku ya pili: Vilifanyika vikao vya kitafiti ambavyo zilisomwa mikhtasari za tafiti iliyo endana na kauli mbiu ya kongamano la mwaka huu, tafiti zilizo andikwa kisomi na kukidhi vigezo vyote vya kielimu hadi zikapasishwa kushiriki katika kongamano hili, zilikua sawa na mistari ya nuru siku zitaendelea kushuhudia katika kila zama, ni ukumbusho kwa atakaye taka kufuata njia ya Mola wake.

Siku ya tatu: Yalipangika mashairi ya wapenzi katika ardhi ya Karbala, kongamano lilipambwa kwa maneno ya mahaba na vielelezo vya utiifu katika vikao vyake, mashairi yalikua yameandikwa kwa maji ya uhai yakisomwa na koo za wafuasi na wapenzi wa hali ya juu wa Zaharaa na baba yake, mme wake, watoto wake na siri iliyo fichika kwake”.

Akamalizia kwa kusema kua: “Shuguli za kongamano zikahitimishwa kwa kuinamia kaburi la bwana wetu Alkafeel (a.s) tukashukuru usimamizi wake, na tukaomba siku hii iwe ni mwanzo wa maandalizi ya kukutana tena kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tukiwa tunaimba kujitolea kwa majemedari miongoni mwa watoto wa Zaharaa walio itikia wito wa Marjaiyya na wakajitolea kwa hali na mali kuinua bendera ya uislamu, wakawa wamefuata njia ya haki na kielelezo cha utukufu hadi itakapo dhihiri haki na kuidhiniwa utawala wa haki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: