Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza kufanya kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya nne.

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kufanya kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) awamu ya nne chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir: ni tunu ya wasii (a.s) na mrithi wa elimu ya Mitume (s.a)), siku ya Juma Tatu mwezi mosi Rajabu 1439h sawa na 19 Machi 2018m.

Makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdul-Hussein Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kongamano hili litakua na mada za kihauza na kisekula na litakua na washiriki wa ndani na nje ya Qatar, tayali wamesha alikwa baadhi ya viongozi wa hauza ya Najafu na walimu wa sekula pamoja na taasisi na vitengo vya serikali katika mikoa ya Iraq ikiwa ni pamoja na (Karbala, Baabil na Najafu), kongamano litakua na vikao viwili cha asubuhi na jioni”.

Kongamano hili litafanyika (1 Rajabu) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (a.s) na litaangazia uhai wa Imamu Baaqir (a.s) na kumuenzi kwa kuonyesha kazi kubwa aliyo fanya ya kupambana na harakati za fikra potofu zilizo dhihiri katika zama zake, na tutaangazia mambo aliyo fanya katika kupambana na harakati hizo kwa wakati.

Akaashiria kua: lengo la kongamano hili ni kufikisha ujumbe kwa kila mfuasi wa Ahlulbait (a.s), aweze kufahamu kiongozi huyu mtukufu namna alivyopambana na fikra potofu wakati ule.

Akaongeza kusema kua: Hakika Imamu Baaqir (a.s) hakuna mnasaba rasmi wa kumkumbuka, ndio maana Atabatu Abbasiyya tukufu imeamua kua inahuisha mnasaba huu mtukufu sawa iwe katika tarehe ya kuvunjwa kwa kaburi lake tukufu (8 Shawwal) au tarehe ya kukumbuka kuzaliwa kwake kwa kufanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s), kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tunatarajia miaka ya mbele tuwe tuna alika watu kutoka nchi nyingi za kiarabu na kiajemi kuja kuhudhuria na kushiriki kwenye hili kongamano.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: