Sayyid Swafi: Najafu bado imedhulumiwa pamoja na urithi mkubwa ilio nao katika kila sekta…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayydi Ahmadi Swafi amebainisha kua: “Nina amini kua Najafu bado imedhulumiwa pamoja na urithi mwingi iliyo nao katika kila sekta, kwa bahati mbaya wakati tulionao hivi sasa unaweza kua wa masikitiko na wala tusiwe na lakufanya zaidi ya kusikitika”.

Ameyasema hayo katika ujumbe wake kwenye hafla ya ufunguzi wa kongamano la kimataifa kuhusu uhuishaji wa kutengeneza historia na kuiandika, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya, chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) lililo anza siku ya Alkhamisi (26 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (15 Machi 2018m) litakalo dumu siku mbili.

Akaongeza kusema kua: “Kwa ujumla historia hutokana na harakati za mwanadamu katika ardhi hii, yale aliyo yafanya kwa hiyari au bila hiyari, hivyo historia ni kukusanya matukio ya watu na kuyaweka mbele ya macho ya watu, au unaweza kusema ni watu waliopo kuangalia yaliyo fanywa na watu walio pita kitamaduni, kielimu, kiujenzi na vitu vingine”.

Akasema kua: “Yawezekana matukio hayo yakawa yanatofautiana sana, unaweza kukuta baadhi ya matukio ya kila siku ambayo hayawakilishi ispokua mtu binafsi na wala hayana umuhimu, na upande mwingine unaweza kukuta matukio makubwa yaliyo sababisha athari kubwa katika jamii nzima, kama vile harakati zilizo fanywa na mitume, waja wema na wanachuoni, au kama vile uvumbuzi wa kielimu ulio badilisha utaratibu wa maisha, au vita zilizo angamiza mamilioni ya watu, au matukio ya kihistoria yaliyo asisi itikadi na mitazamo na yakafanyika yaliyo fanyika kutokana na mitazamo hiyo”.

Sayyidi Swafi akaendelea kusema: “Kwa kweli historia yetu ya kiislamu imejaa matatizo mengi, tunapo angalia historia tunakuta baadhi ya matukio yalitikisa umma, na yalijirudia, matukio hayo ukiyaangalia yalikua yanahusu mtu binafsi, kisha yakaendelezwa hadi yakawa yanawakilisha itikadi, hili ni tatizo la kihistoria, ukisoma historia vizuri kama tutakavyo ona kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu katika kongamano hili, kuna vipengele vya historia yatupasa tuviangalie vizuri, sio kwamba vinahusu watu peke yake, au visa vya kawaida bali yatupasa kuchukua mazingatia”.

Akabainisha kua: “Sio kila tukio la kihistoria tulipite haraka haraka, bali baadhi ya matukio ya kihistoria yalizaa mambo mazuri au mabaya, jambo muhimu ni kwamba baadhi ya matukio ya kihistoria yalitengeneza mtazamo na itikadi ambayo ina athari katika maisha yetu, bila shaka kuchambua haki na isiyo kua haki, ukweli na uongo katika matukio hayo sio jambo jepesi kama hatuna vielelezo, hususan tunapo kosa ushahidi wa kimaandishi baadhi ya wakati, ua jambo lenyewe linatoweka katika vitabu kama tunavyo shuhudia katika baadhi ya vitabu vya historia”.

Sayyid Swafi akaashiria kua: “Iraq na Najafu yalikua maeneo ya kijografia muhimu, kutokana na mambo ya kihistoria yaliyo fanyika katika sekta ya idikadi, elimu, siasa na lugha, jambo hili linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Baharul-Uluum ya kutengeneza historia na kuiandika, lilipaswa kua sio la mwanzo, hakika jambo la historia limesisitizwa sana na sheria tukufu, kiongozi wa waumini (a.s) anasema katika wasia wake kwa mwanaye Imamu Hassan: (Uhuishe moyo wako kwa mawaidha na ifishe kwa kuyapuuza…) hadi alipo sema: (Ujulishe habari za watu waliopita na uukumbushe yaliyo wapata walio kua kabla yako na upite katika nyumba zao na athari zao…) hadi mwisho wa maneno yake (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Sisi tunafanya utafiti kwa kuangalia mitazamo na fikra zilizo andikwa na ndugu zetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atuwafikishe sote, na kongamano hili liwe ni msingi wa kongamano lijalo litakalo fanyika kuusifu mji huu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: