Kwa matokeo bora ya kilimo: Shirika la uchumi Alkafeel lashiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo na lasisitiza kua, sisi tunamsaidia mzalishaji na tunamlinda…

Maoni katika picha
Bega kwa bega na mashirika makubwa ya kitaifa na kimataifa, shirika la uchumi Alkafeel lashiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo awamu ya kumi na siku ya mti, yanayo simamiwa na wizara ya kilimo ya Iraq, chini ya kauli mbiu isemayo: (Tuifanye Iraq kua kijani kibichi) kuanzia (14-21 Machi 2018m) katika uwanja wa makumbusho ya kimataifa Bagdad.

Ushiriki wao katika maonyesho haya ulikua na faida kubwa katika sekta zote ya pembejeo za kilimu na ufugaji, matawi yake yalionyesha bidhaa za mfano kutoka katika mashamba ya Khairaat Abulfadhil Abbasi (a.s), kama vile: matango, bilinganya, tomate (nyanya) na mengineyo, ambazo ni bidhaa bora kabisa zinazo limwa kienyeji bila kutumia kemikali zenye madhara kwa watumiaji, jambo lililo ziweka kwenye nafasi ya kwanza ya ubora katika soko la Iraq.

Hali kadhalika walikua wanaonyesha bidhaa mbalimbali wanazo zalisha kupitia folda na vipeperushi, vinavyo elezea miradi tofauti inayo endeshwa na shirika hili, kama vile mradi wa Alkafeel wa mashine za kutotolea mayai na uzalishaji wa vifaranga vya kuku wa mayai na wa nyama.

Wasimamizi wa tawi hili wamesema kua: ushiriki wetu ulikua na tija, tumeweza kufikisha ujumbe kua Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia miradi hii na mingine ni msaada mkubwa kwa wazalishaji, jambo ambalo matunda yake yataonekana katika uchumi wa taifa, na kuirudisha Iraq katika nafasi yake ya zamani kama taifa linalo zalisha, na sio linalo tumia tu (bidhaa kutoka nje), hakika tuna rasilimali nyingi iwapo zikitumika vizuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: