Semina za kumtambua mwalimu mwenye mafanikio katika taauma ya uwalimu…

Maoni katika picha
Idara ya mahusiano na vyuo (ofisi ya harakati za shule) chini ya kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya tukufu, inaendesha semina za kumtambua mwalimu mwenye mafanikio, zinazo fanyika katika ofisi za malezi za mikoa ya Iraq, hivi karibuni wamemaliza semina ya kumi ambayo ilikua ni hitimisho la semina zilizo tangulia, na ilikua na washiriki 33 kutoka katika shule na vituo vya malezi kwenye miji iliyopo ndani ya mkoa wa Baabil.

Ustadh Azhar Rikabi katika ujumbe aliotoa wakati wa kufunga semina, aliwapongeza washiriki kwa kufanikisha semina hiyo, na akaonyesha matumaini ya kunufaika kutokana na semina hiyo, jambo litakalo changia kuboresha kiwango cha elimu ya Iraq, akathibitisha kua Atabatu Abbasiyya inaendelea kufanya semina za aina hii, na watajitahidi kuwafikia walimu wengi kiasi itakavyo wezekana.

Washiriki wa semina kupitia kiongozi wao bi Laila Jawaad walisema kua: Hakika hatuna maneno yanayo weza kubeba wingi wa shukrani zetu, shukrani za pekee ziiendee Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake, kwa kutupa semina hii ambayo imetuongezea fahari, kwa kukutana na nyuso hizi tukufu na kuchota katika elimu zao na kuanza safari ya kuelekea katika utekelezaji wa ujumbe tuilo wajibishwa kuufikisha, hakika tumejifunza mengi katika semina hii, tutayafanyia kazi na kuhakikisha tunamfurahisha kila mtu katika mkoa wa Baabil kwa kuboresha kiwango cha elimu.

Mwishoni mwa mkutano huo, washiriki wa semina wakapewa vyeti, na wakaendelea kueleza shukrani zao kwa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kuwapa semina hii ambayo ina mchango mkubwa wa kuongeza kiwango chao cha elimu na kuwawezesha kupambana na changamoto mpya zinazo zuka kila siku katika maisha yao jambo ambalo litasaidia kuboresha kiwango cha elimu.

Kumbuka kua semina hii ilikua na vipengele vingi, vinavyo lenga kuinua kiwango cha uwezo wa walimu, na kuwafanya waweze kuboresha selibasi za masomo, kutokana na maendeleo ya elimu na njia za kisasa katika kufikisha maarifa kwa mwanafunzi kwa njia nyepesi na sahihi, na walionyeshwa mambo mapya yanayo zuka pamoja na changamoto zake, semina hii ilikua ni ya siku tatu, masomo yalijikita katika mambo yafuatayo:

  • 1- Kufuatanisha vitendo.
  • 2- Kusoma harakati.
  • 3- Kutumia maneno ya kimaendeleo ya wanadamu katika ufundishaji.
  • 4- Njia mpya za ufundishaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: