Kuanza kwa kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) la mwaka wa nne

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s) uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, asubuhi ya Juma Tatu (1 Rajabu 1439h) sawa na (19 Machi 2018m) wamefanya kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s), ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), lenye kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) ni tunu ya wasii (a.s) na mrithi wa elimu ya Mtume (s.a.w.w)).

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, halafu ukaibwa wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Shekh (Swalahu Karbalai) rais wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, akabainisha kua: “Tunatoa pongezi kwa ndugu zetu wasimamizi wa kongamano hili, na tunawapongeza kwa kuzaliwa Imamu wetu Baaqir (a.s) mtu aliye fanya haraka kupata elimu ya Aali Muhammad (a.s), kila sifa nyema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametupa neema ya wilaya, na akatuongoza kwa dalili za wazi tuwafuate Ahlulbait (a.s), hususan Imamu wetu wa zama ambaye roho zetu na roho za waumini wote zipo tayali kujitolea kwa ajili yake, kwa ajili ya kufuata njia ya haki, leo tunahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s) tunahuisha utiifu wetu kwake na kufuata mwenendo wake. Kinacho fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa makongamano na mikutano chini ya usimamizi wa kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, na ili kongamano likamilike katika pande mbili: Upande wa kumtambua Imamu ambao hauna kikomo, na upande wa kuitambua nadhariyya. Jambo hili linahitaji maandalizi, katika zama hizi tunahitaji kuongeza juhudi ya kumtambulisha Imamu Baaqir (a.s) pamoja na matatizo tunayo yapitia”.

Akaongeza kusema kua: “Tunawaomba watafiti wa kisekula na wanachuoni wa dini waandike tafiti kuhusu Imamu Baaqir (a.s), wautambulishe utukufu wake, hakika yeye ndio muasisi wa mwanzo wa madrasa ya Ahlulbait (a.s) na sisi leo tunajulikana kwa jina la madrasa hiyo, haifai tuzembee katika hili”.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awawezeshe wasimamizi wa kongamano hili, na awaimarishe katika mwenendo wa Ahlulbait (a.s).

Kisha kongamano likaingia katika awamu ya kikao cha kitafiti cha asubuhi, kilicho simamiwa na Dokta Karim Hussein Naaswih, mshauri wa taaluma katika kituo cha kimataifa cha Ameed, kikaanza kwa kusikiliza utafiti ulio wasilishwa na Shekh Harith Dahi usemao (Kupambana kwa Imamu Baaqir (a.s) dhidi ya fikra potofu).

Kikao kilishuhudia maoni, maelezo na maswali mengi kutoka kwa wahudhuriaji, mtoa mada alijibu na kufafanua palipo hitaji ufafanuzi.

Fahamu kua ufunguzi wa kongamano hili ulikua na mahudhurio makubwa ya viongozi wa dini na kisekula pamoja na idadi kubwa ya watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: