Kufanyika kwa maukibu (matembezi) rasmi ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kwa ajili ya kuomboleza kuuawa kishahidi kwa Imamu Ali Haadi (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya siku ya Juma Tano (3 Rajabu 1439h) sawa na (21 Machi 2018m), yamefanyika matembezi rasmi ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, yakiwa na ushiriki mkubwa wa viongozi na watumishi wa Ataba hizo, kwa ajili ya kuhuisha msiba huu na kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Matembezi hayo yalianzia katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), yakapita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na kuelekea hadi katika malalo ya Abul-Ahraar Imamu Hussein (a.s), kisha wakafanya majlis ya matam ndani ya haram hiyo tukufu, matembezi haya yamepambwa na kaswida pamoja na maneno ya kuomboleza yaliyo bainisha ujumbe wake na kuonyesha mapenzi ya watumishi wa Ataba mbili tukufu na kushikamana kwao na mwenendo wa Ahlulbait (a.s) pamoja na njia aliyo pita Imamu Ali Haadi (a.s).

Kwa upande mwingine mji mtukufu wa Karbala una hali ya huzuni kutokana na tukio hili linalo umiza mioyo ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Kumbuka kua Ataba tukufu za Karbala hufanya matembezi rasmi katika kumbukumbu za vifo au uzawa wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: