Kutokana na shambulio la kinyama iliyo fanyiwa: Makumbusho ya Alkafeel yaonyesha umbo la kubba ya Abulfadhil Abbasi (a.s) linalo onyesha athari za kushambuliwa…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kukubuka uadui mbaya ulio fanyiwa Ataba tukufu za Karbala, kufuatia maandamano ya Shaabaniyya matukufu ambayo kumbukumbu yake inaangukia katika siku hizi kwa mujibu wa kalenda ya miladi, na kwa ajili ya kukumbuka unyama wa uadui huo na chuki dhidi ya malalo matukufu ikiwemo malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kubba tukufu na sehemu zingine za haram zilishambuliwa na kila aina ya siraha.

Makumbusho ya Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika kumbukumbu ya maandamano ya Shaabaniyya tukufu ya mwaka wa pili, yanayo simamiwa na kituo cha utamaduni cha kimataifa chini ya ulezi wa Atabatu Husseiniyya tukufu na yenye kauli mbiu isemayo: (Damu tukufu ya waandamanaji wa Shaabaniyya imezaa matunda ya ushindi wa Hashdi watukufu).

Kiongozi wa kitengo cha makumbusho Ustadh Swadiq Laazim ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Maonyesho yanafanyika katika eneo lililo funikwa la katikati ya haram mbili tukufu, vimeshiriki vikundi vingi katika maonyesho haya, kuna kubba kubwa ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) linalo onyesha athari ya kushambuliwa kwa kupigwa na mabomu, hali kadhalika zinaonekana tofali zilizo haribika baada ya kushambuliwa, pia kuna vielelezo vingine vinavyo thibitisha madhara yaliyo patikana baada ya kushambuliwa, na kuna picha nyingi zinazo onyesha hali ilivyo kua baada ya shambulio hilo.

Ustadh Kamal Basha rais wa kituo cha utamaduni cha kimataifa amesema kua: “Hakika mateso waliyo pata raia wa Iraq wakati wa utawala wa Baathi, hayaja wahi kuwapata watu wengine wowote, hakuna mtu muovu zaidi ya aliye kua kiongozi wa Iraq, aliua raia wake, akabomoa taifa lake na akadhalilisha utu wa wairaq, kutokana na mateso hayo, ikapatikana fikra ya kufanya maandamano haya ambayo wairaq hawata sahau kilicho watokea, tutaendelea kuyaenzi kwa ajili ya kuheshimu haki ya mashihidi walio jitolea kwa ajili ya Iraq”.

Kumbuka kua katika kongamano hili yameshiriki makundi mbalimbali yenye uhusiano na maandamano ya Shaabaniyya matukufu, pamoja na makumbusho ya Alkafeel, taasisi ya mashahidi, taasisi ya wafungwa wa kisiasa, taasisi ya Nabaa ya utamaduni na habari, pamoja na jopo la watalamu kutoka mikoa mbalimbali ya Iraq, wanaonyesha picha za mnato zinazo onyesha jinai za serikali iliyo ondolewa madarakani (ya Sadam), na kuna mabango yanayo onyesha dhulma walizo fanyiwa watu wa Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: