Usiku wa Ijumaa ya kwanza katika mwezi wa Rajabu Aswabu: Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) yafurika mazuwaru, na watumishi wake watumia uwezo wao wote katika kuwahudumia…

Maoni katika picha
Hakika ni siku ya Alkhamisi ya kwanza na usiku wa Ijumaa wa kwanza wa mwezi mtukufu wa Rajabu, na huitwa usiku wa Raghaaibu, ni usiku wenye rehma nyingi mno, unaheshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu na huongeza thawabu mara dufu, waumini wamezowea kutumia siku hii kwa kufanya ibada katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na katika eneo la uwanja wa katikati ya malalo mahiri hayo matakatifu, kwa ajili ya kuongeza msimamo na kujikumbusha subira katika haki na kunusuru dini.

Mji mtukufu wa Karbala tangu asubuhi unashuhudia makundi makubwa ya watu wanao ingia katika mji huo, kutoka ndani na nje ya Karbala pia hadi kutoka nje ya Iraq, kilele cha mafuriko ya watu kilikua jioni ya siku ya Alkhamis, nao watumishi wa Ataba mbili tukufu wametumia uwezo wao wote kuimarisha ulizi na kutoa huduma bora zaidi na kuwawezesha kufanya ziara na ibada kwa urahisi na utulivu.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na juhudi zao tukufu na kufuatia utaratibu wao wa kutoa huduma ambao huutekeleza kila usiku wa Ijumaa na mchana wake, wametumia uwezo wao wote kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru watukufu na kuwafanya waweze kufanya ziara na ibada zao zingine kwa amani na utulivu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: