Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada yatangaza kuongeza muda wa kupokea mada za kitafiti zitakazo shiriki katika shindano…

Miongoni mwa sehemu za kongamano
Kamati ya maandalizi ya shindano la kitafiti litakalo fanyika sambamba na kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, litakalo fanyika mwanzoni mwa mwezi ujao wa Shabani chini ya kauli mbiu isemayo (Tumepigana kwa utukufu wa Hussein (a.s) na tumeshinda kwa utukufu wa fatwa) imetangaza kuongeza muda wa kupokea mada za kitafiti zitakazo shiriki hadi tarehe 10 Rajabu 1439h, badala ya muda wa zamani, kwa ajili ya kutoa nafasi zaidi kwa wanao penda kushiriki, watume tafiti zao kupitia anuani za barua pepe zifuatazo: (rabee@alkafeel.net / almaaref@alkafeel.net / inahj.org@gmail.com).

Kamati imebainisha kua mabadiliko yanahusu ukomo wa tarehe ya kupokea tafiti peke yake, kanuni na masharti mengine yataendelea kua kama yalivyo, ambayo ni:

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kutolewa na watu wengine.
  • 2- Uandikwe kwa kufuata misingi na kanuni za kielimu.
  • 3- Usiwe chini ya kurasa (15) na usizidi kurasa (30) na uandikwe kwa hati ya (Arabic simplified) maandishi yake yawe na ukubwa wa saizi (14) na uhifadhiwe kwenye (CD).
  • 4- Usizidi maneno (300) na uambatanishwe na muhtasari wake.
  • 5- Utafiti wowote ambao hautakidhi vigezo hautakubaliwa, pia utafiti utakao kosa wasifu (CV) ya muandishi hautakubaliwa.
  • 6- Tafiti zote zitumwe pamoja na mihtasari yake ikiambatana na wafisu wa muandishi, picha, namaba ya simu na anuani ya barua pepe, kupitia anuani ya barua pepe au zipelekwe moja kwa moja katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatyu Abbasiyya tukufu, au katika taasisi ya Uluum Nhaju-Balaghah katika Atabatu Husseiniyya tukufu, kabla ya tarehe (10 Rajabu 1439h) fahamu kua tayali zawadi za washindi wa tatu wa mwanzo zimesha andaliwa, kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: (1,500,000) milioni moja na nusu dinari za Iraq.

Mshindi wa pili: (1,000,000) milioni moja dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu (750,000) laki saba na elfu hamsini dinari za Iraq.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia barua pepe zifuatazo:- rabee@alkafeel.net /

almaaref@alkafeel.net / inahj.org@gmail.com.

Au moja ya namba za simu zifuatazo: (07723757532 / 07728243600 / 07815016633).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: