Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa warsha ya kuwajenga uwezo wa kuandaa mpango mkakati kwa marais wa vitengo vyake…

Sehemu ya warsha
Kwa ajili ya kuwajengea uwejo wa kiutendaji ili kuboresha huduma zao, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia ofisi ya katibu mkuu na kitengo cha malezi na elimu ya juu wameratibu warsha kuhusu kuandaa mpango mkakati, iliyo ongozwa na Profesa Hamza Muhanna msaidizi wa kitengo cha sekula katika chuo kikuu cha Suhaar nchini Oman, ambayo imewahusisha marais wavitengo vya Ataba na wasaidizi wao.

Warsha hii imefanyika katika ukumbi wa jengo la Imamu Mahdi (a.s) ni moja ya warsha na nadwa za kujenga uwezo ambazo hufanywa na Atabatu Abbasiyya kwa watumishi wake au marais wa vitengo, kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kiutendaji na kila mtu hupewa masomo yanayo endana na kazi yake.

Warsha ilikua na mijadala na maelezo ya muhimu kuhusu mipanga mikakati ya marais wa vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, pia walijadili sana mazingira kielimu pamoja na mazingira ya kazi, pia walijadili dira, utume na malengo pamoja na misingi ya Ataba tukufu na hatua za kuandaa mpango mkakati.

Profesa Hamza Muhanna amebainisha kua: “Warsha hii inahusu kuweka mpango mkakati ambao utatuwezesha kujua tunataka kua vipi? Na vipi tutafikia hapo? Mpango mkakati unahatua nyingi zinazo takiwa kufatwa, kwa ufupi tunaanza kuchambua muundo wa taasisi wa ndani na nje, kisha tunaangalia lengo kuu na dira yake, wanataka kua vipi, baada ya kubaini dira yao ndipo tunaiwekea malengo yanayo weza kutekelezwa na kutufikisha mahala fulani ndani ya muda fulani kutokana na mpango mkakati, malengo hayo pia huyagawa katika malengo ya awali na malengo ya pili, kwa kuyaowanisha na mkakati, baada ya kumaliza kutengeneza mpango mkakati hutakiwa kutengeneza mpango kazi, (vitu hivyo huenda pamoja), husaidia kuwafanya watumishi wote kuanzia wa ngazi ya chini kabisa hadi wa ngazi ya juu wafanye kazi kwa mpangilio, lazima kuainisha malengo, shughuli na matokeo kwa kufuata muda ulivyo pangwa katika mpango mkakati, njia hii husaidia taasisi zisipoteze muda na kuzifanya zifikie malengo yao, huu ni utaratibu wa kimataifa ambao hutumiwa na taasisi ndogo na kubwa”.

Washiriki wamesisitiza umuhimu wa kufanyika kwa ratiba za aina hii kwa ajili ya kuwajengea uwezo, kwa sababu zina mchango mkubwa wa kuboresha kazi, pia zinachangia kuongeza uwezo wa watumishi, bila kusahau umuhimu wake katika kuongeza uwezo wa mtu binafsi na kumfanya aweze kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, na zinasaidia kufuatilia maendeleo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: