Maandalizi ya maonyesho makubwa ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanaendelea…

Maoni katika picha
Maandalizi ya maonyesho makubwa yatakayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, yatakayo husisha miradi yake ya kitamaduni, kiuchumi na kiutumishi, yanayo tarajiwa kuanza asubuhi ya Juma Mosi ijayo (13 Rajabu 1439h) sawa na (31 Machi 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Miradi yetu inashajihisha uwezo wa taifa), yatafanyika sambamba na kumbukumbu za kuzaliwa kwa simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda Ali bun Abu Twalib (a.s) na ufunguzi wa moja wa miradi ya Ataba tukufu ambao ni kituo cha kibiashara cha Afaaf.

Maonyesho hayo yatadumu siku kumi, yatafanyika katika uwanja wa kituo cha Afaaf, asilimia kubwa ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vitashiriki, kwa ajili ya kuwaonyesha wananchi na mazuwaru watukufu pamoja na taasisi za serikali na zisizo kua za serikali maendelea na shughuli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa upande mwingine kwa ajili ya kuonyesha uzowefu wao ulio wawezesha kupata maendeleo ambao yanachuana na mafanikio ya kimataifa.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maonyesho haya na mkuu wa kituo cha uchapishaji Alkafeel, ambao ndio wenye jukumu kubwa la maandalizi na kutoa matangazo, Ustadh Muhammad Aali Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki mara nyingi katika mahafali mbalimbali za ndani na nje, vitengo vyake vilikua vinashiriki kutokana na aina ya ushiriki unao hitajika, lakini ushiriki wa aina hii hauja wahi kutokea, maonyesho yanasimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na washiriki ni vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo hili linatufanya tuongeze umakini zaidi katika kufanya maandalizi, ili maonyesho haya yawe bora zaidi na yenye muonekano mzuri unao endana na hadhi ya Ataba tukufu, pamoja na bidhaa inazo tengeneza zitakazo shiriki kwenye maonyesho hayo”.

Akaongeza kusema kua: “Kamati ya maandalizi imesha fanya vikao mara nyingi na washiriki wa maonyesho na kupata picha halisi ya vitu vitakavyo onyeshwa, ndipo tukakadiria ukubwa wa eneo la kila tawi na namna ya kujenga sehemu yao kulingana na vutu watakavyo onyesha, kwa namna ambayo vitakua na muonekano mzuri wa kuvutia, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s) maonyesho haya yatakua mfano bora katika kila sekta”.

Kumbuka kua watakao shiriki katika maonyesho haya ni: (Shirika la usalama Alkafeel, kitengo cha mgahawa pamoja na kitengo cha nidham, shirika kuu la uchumi Alkafeel pamoja na shirika la Aljuud, shirika la maji Alkafeel pamoja na vitengo vingine vya mashirika, shirika la bendera ya kimataifa, kitengo cha miradi ya kihandisi, kitengo cha zawadi na nadhiri, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kitengo cha elimu na utamaduni pamoja na maahadi ya watalamu ya kujenga uwezo na kukuza vipaji, idara ya Intanet, kituo cha uchapishaji Alkafeel, kitengo cha makubusho Alkafeel, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, idara ya kunufaika na mitambo, shirika la Nurul-Kafeel, hospitali ya Alkafeel, kitengo cha utumishi, uongozi wa kituo cha Afaaf, kiwanda cha Ataba tukufu cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi, chuo kikuu cha Ameed, mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: