Mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) watengeneza mchoro wa mazazi matukufu katika mlango wa kibla wa malalo yake tukufu…

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanao fanya kazi katika vitalu vya Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi, wametengeneza mchoro kwa kutumia maua ya rangi nyeupe na kijani usemao: Ali kazaliwa ndani ya Kaaba (Aliyyu Waliidul-Ka’aba), mchoro huo wameuweke mbele ya mlango wa kibla wa haram tukufu ya malalo ya mwanaye Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mchoro huo una urefu wa mita nne na upana wa mita mbili, sehemu hiyo imepambwa na rangi ya maua ya banafsaji, pamezungushiwa bango kuanzia chini, pametengenezwa kwa kufuata vipimo maalumu, rangi za maua zimepangwa kutokana na eneo lenyewe, kiasi kwamba kwa ujumla pamekua na muonekano mzuri, kazi hiyo inaonyesha umakini wa utendaji na uhodari wa upangiliaji wa rangi, kila anaye angalia sehemu hiyo moyo wake unafurahi, na inamuongezea furaha zaidi katika siku hizi tukufu za sherehe katika mji mtukufu wa Karbala.

Mazuwaru (watu) wengi wanaokuja kufanya ziara katika haram hii tukufu wanasimama kwa muda mrefu wakiangalia kazi iliyo fanywa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuburudisha macho yao pamoja na kupata harufu nzuri ya maua hayo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: