Mwezi kumi na tatu Rajabu ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) ndani ya Kaaba tukufu…

Maoni katika picha
Alizaliwa katika haram ya Mwenyezi Mungu na amani yake*** Ni nyumba ambayo uwanja wake ni msikiti.

Akiwa mweupe msafi wa nguo zake tukufu*** Ametukuka mzaliwa na katukuka mzazi wake.

Hajapata bebwa mtukufu kama yeye*** Ispokua mtoto wa Amina Nabii Muhammad.

Miongoni mwa mambo muhimu yaliyo tokea katika Kaaba tukufu ni tukio la kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s) ndani ya nyumba hiyo tukufu, siku ya Ijumaa (13 Rajabu) miaka thelathini baada ya mwaka wa tembo, ni wazi kua tukio hili ni alama ya wazi kuhusu utukufu wake (a.s), utukufu huo katunukiwa na Mwenyezi Mungu mtukufu na hajapata kutunukiwa mwingine yeyote zaidi yake, kwani hajawahi kuzaliwa ndani ya Kaaba mtu yeyote kabla yake wala baada yake, jambo hili limethibitishwa na wana historia wote.

Kutoka kwa Said bun Jubairi anasema: Yazidi bua Qa’nab anasema: Nilikua nimekaa na Abbasi bun Abdulmutwalib pamoja na kundi la watu wa Abdul-uza pembezoni mwa nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu, tukamuona Fatuma bint Asadi mama wa kiongozi wa waumini (a.s) anakuja, na alikua na mimba ya miezi tisa, akiwa amepatwa na uchungu, akasema: Ewe Mola mimi nakuamini na ninaamini mitume wako na vitabu vyako, ninasadikisha maneno ya babu yangu Ibrahim kipenzi wako, hakika yeye ndiye aliyejenga nyumba hii, kwa haki ya aliye jenga nyumba hii na haki ya mtoto aliye tumboni mwangu nakuomba unifanyie wepesi uzaaji wangu.

Yazid bun Qa’nab anasema: Tukaona nyumba imejifungua na Fatuma akaingia na kutoweka machoni kwetu, na ile sehemu aliyo ingilia ikajifunga, tukaenda kufungua mlango lakini haukufunguka, tukatambua kua hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu, akatoka baada ya siku nne akiwa amembeba kiongozi wa waumini (a.s), akasema: Nimetukuzwa kushinda wanawake wote walio tangulia, kwa sababu Asia bint Muzaahi alimuabudu Mwenyezi Mungu mtukufu kwa siri katika zama ambazo mtu anaye muabudu Mwenyezi Mungu alikua anateswa, na Maryam bint Imraan alitikisa mtende mbichi kwa mikono wake ndipo akadondoshewa tende mbivu alizo kula, na mimi nimeingia katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na nimekula matunda ya peponi, na nilipo taka kutoka nimesikia sauti ikiniambia: Ewe Fatuma mwite! Ali, mtoto huyu anaitwa Ali, na Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: nimetoa jina lake katika jina langu, na nimemfundisha adabu inayo tokana na mimi, na nimempa elimu itokanayo na mimi, yeye ndiye atakaye vunja masanamu katika nyumba yangu, na ataadhini juu ya nyumba yangu, atanitakasa na kuniabudu, amefaulu atakaye mpenda na kumtii, (1) na ameangamia atakaye mchukia na kumuasi.

Jambo muhimu la kuzingatiwa hapa ni kwamba; utukufu alio pata Imamu Ali (a.s) wa kuzaliwa ndani ya Kaaba, hauja wahi kupatikana kwa mwanadamu yeyote, Ali ni wa kwanza kuzaliwa ndani ya Kaaba tukufu na hata zaliwa humo yeyote baada yake, hiyo ni heshima maalumu aliyo pewa na Mwenyezi Mungu mtukufu.



------------------

  • (1) Biharul-Anwaar cha Allamah Majlisi jz: 35/uk: 8.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: