Mawakibu za kuomboleza zinaendelea kumiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhuisha kifo cha mtukufu wa Twafu bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Juma Tatu (15 Rajabu 1439h) sawa na (2 Aprili 2018m), Mawakibu za kuomboleza zimeendelea kumiminika katika kaburi la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kutoa pole kwa Imamu wa Zama (a.f) na kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha bibi Zainabu bint Ali bun Abu Twalib (a.s).

Mawakibu za kuomboleza zimezowea kila mwaka asubuhi ya mwezi 15 Rajabu huja katika malalo hizi kutoa pole na kuhuisha msiba huu, hivyo leo zimeshuhudiwa mawakibu (makundi ya watu) wakiwa wamevaa nguo nyeusi huku wakiimba kaswida zinazo elezea misiba aliyo pata bibi Zainabu (a.s).

Chini ya utaratibu ulio wekwa na kitengo cha Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, Mawakibu zilikua zinaanza kuingia katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kisha zinakwenda katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s), wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na wanafanya majlis ya kuomboleza katika haram hiyo, amani iwe juu ya sauti ya Hussein na mtazamo wake, na juu ya pumzi zake pamoja na dada aliye linda harakati yake.

Kumbuka kua bibi Zainabu (a.s) alifariki mwaka wa (62h) baada ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa vita ya Karbala, anamajina mengi, linalo julikana zaidi ni Jabali la Subira, ana haki ya kuitwa hivyo, kwani alishuhudia vita ya Twafu na akavumilia machungu ya kuuawa kwa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na mambo yaliyo mpata baada ya vita hiyo ikiwa ni pamoja na kufanywa mateka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: