Katika mahudhurio makubwa: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kongamano la kitamaduni Amirul Mu-minina (a.s) katika mji wa Karkal India…

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyo jaa heri, rehma na baraka, zinazo tokana na kuwapenda Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Amirul Mu-minina Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), na chini ya kauli mbiu isemayo: (Amirul Mu-uminina (a.s) ni wa mwanzo katika wenye kuabudu na mwenye zuhudi zaidi katika wenye zuhudi), Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kongamano hili kwa mwaka wa sita mfululizo lililo anza asubuhi ya leo Alkhamisi (18 Rajabu 1439h) sawa na (05 Aprili 2018m) katika mji wa Karkal India na kushiriki Ataba mbili tukufu ya Husseiniyya na Askariyya, chini ya uwenyeji wa hauza ya Ithna Ashariyya na litaendelea kwa muda wa siku tatu.

Hafla ya ufunguzi ilipambwa na shughuli ya kupandisha bendera za kubba mbili tukufu ya Imamu Hussein na ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi pamoja na Maimamu wawili Askariyyaini (a.s) katika lango la kuingia hauza, kisha wahudhuriaji wakelekea katika uwanja wa katikati ya hauza kwa ajili ya kuanza kwa ratiba za kongamano, lililo pata mahudhurio makubwa ya wanachuoni wa dini na sekula pamoja na idadi kubwa ya wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka ndani na nje ya mji huu, baada ya Qur’an ya ufunguzi iliyo somwa na msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Liith Abedi, ulifuata ujumbe wa Ataba tukufu za Iraq ulio wasilishwa kwa niaba yao na rais wa ujumbe wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika Imamu Ali (a.s) ni hema lililo tukusanya wote, pamoja na umbali na kutofautiana kwa lugha mitazamo na madhehebu, kilicho tukusanya na kutufanya kua kitu kimoja ni mapenzi ya kibinadamu na akili tukufu…”.

Kisha ukafuata ujumbe wa wenyeji wa kongamano ulio wasilishwa na Shekh Nasir Mahadi Muhammadi ambaye alibainisha kua: “Leo tunawageni watukufu kwetu, wamekuja kutoka nchi kipenzi ya Iraq, wanawakilisha Ataba tukufu, siku hii ya leo inaumaalumu rasmi tofauti na siku zingine, tunajivunia kuwahudumia watumishi wa Ataba tukufu za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), hakika mji wetu umenawirika kwa kupata wageni hawa, hii inatokana na baraka za Maimamu (a.s)…”.

Kisha ukafuata ujumbe kutoka kwa Ahlu Sunna wa mji wa Karkal ulio wasilishwa na Shekh Salim Aarif.

Halafu ukafuata ujumbe wa watu wa mji wa Lahlah Daru ulio wasilishwa na rais wa baraza la wanachuoni wa mji huo Shekh Nadhir Ahmadi Sharifu.

Pia kulikua na ujumbe wa rais wa Jumuiya ya Imamu Swahibu Zamaan (a.f) ulio wasilishwa na Shekh Swadiq Balaghi.

Na mwisho kabisa ulikua ujumbe wa wafuasi wa Sufi katika mji huu, ulio wasilishwa na Shekh Muhammad Baaqir Shaaha, ambaye alisisitiza kua: “Hakika Imamu Ali (a.s) ni wa watu wote, kama Mwenyezi Mungu mtukufu alivyo mteua Mtume Muhammad (s.a.w.w) kwa ajili ya watu wote, na Amirul Mu-uminina ukizingatia kua ni wasii wake, na yeye ni wa watu wote, na ndiye mkamilishaji wa ujumbe wa dini ya Muhammad, hivyo alikua ni kielelezo katika uadilifu na ubinadamu, kama alivyo sema katika kauli yake mashuhuri pale alipo muambia Maalik Ashtar: (Hakika watu wako makundi mawili, imma atakua ndugu yako katika dini au ndugu yako katika uumbwaji) kauli hiyo ni mwongozo kwa kila anayetaka kujiepusha na ubaguzi unao vunja umoja wa watu”.

Hafla ilipambwa na kaswida mbalimbali mwisho wakaswali swala ya jamaa iliyo ongozwa na Sayyid Ibrahim Fadhil kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, halafu wakagawa chakula cha tabaruku kilicho pewa jina la Amirul Mu-uminina (a.s) kwa wenyeji na wageni, pia wageni kutoka Ataba tukufu wakapewa zawadi na wenyeji wa kongamano hili Hauza ya Ithna Ashariyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: