Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chahitimisha maonyesho ya turathi zetu utambulisho wetu ya mwaka wa kwanza.

Maoni katika picha
Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya leo Ijumaa (19 Rajabu 1439h) sawa na (6 Aprili 2018m) kimehitimisha maonyesho ya turathi zetu utambulisho wetu.

Hafla ya kufunga maonyesho hayo imefanywa ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s), ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Mustwafa Hamdani, ikafuatiwa na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha ukaibwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Halafu ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya ulio wasilishwa na Mheshimiwa Shekh Swalahu Karbalai, alizungumzia umuhimu wa turathi, akaonyesha kua ni moyo wa umma na zana ya kutengeneza jamii, akasisitiza umuhimu wa kukusanya turathi kwa ajili ya maendeleo ya umma na kufikia malengo yake, na akaonyesha umuhimu wa turathi zetu za kiislamu hasa za hapa Iraq, tena katika miji miwili, mji wa Kufa na Hilla, miji ambayo imetoa elimu mbalimbali kwa muda wa miaka elfu moja na mia moja, na mwisho akawatakia mafanikio watu wote wanao fanya kazi ya kuhuisha turathi, akakishukuru kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kwa kufanya maonyesho haya.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa wadau na wafadhili wa uhuishaji wa turathi, ulio wasiliswa kwa niaba yao na Mhakiki Dokta Mudharu Hilliy ambaye alisema kua: hakika Atabatu Abbasiyya tukufu haijarudi nyuma katika kuhuisha turathi, kwa kufanya makongamano, nadwa na kutuma wataalamu wa fani hiyo katika kila kona ya Iraq kwenye maktaba za umma na binafsi kwa ajili ya kutafuta turathi. Aliyasema hayo katika ujumbe alio toa kwenye hafla ya kufunga maonyesho ya turathi zetu ndio utambulisho wetu, yaliyo simamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kisha ukafuata ujumbe wa kamati ya majaji wa shindano la picha za mnato (photography) pamoja na kutangaza majina ya watu walio faulu, ulio wasilishwa na Ustadh Haadi Najari rais wa jumuiya ya wapiga picha ya Iraq, alisema kua: Sina cha kusema zaidi ya kuushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kutokana na kujali kwao sekta ya turathi, nitazungumzia kidogo kuhusu picha za mnato (photography), sasa hivi picha hizo ndio lugha ya kimataifa na wala haihitajii kushereheshwa, uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unajali sekta hii kwa sababu wanafahamu umuhimu wake, nchi za jirani hawaruhusu kutengeneza filamu ispokua lazima kuwe na sehemu ya turathi zao ndani ya filamu hiyo, jambo hili ni muhimu sana kwa ajili ya kujenga uwelewa kwa jamii nzima.

Akafafanua kua: “Kuhusu picha za mnato (photography), tunakuta kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilifanya kongamano maalum kuhusu picha za mnato, tunafurahi kupewa majukumu na Atabatu Abbasiyya kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, mimi na Ustadh Abdullahi Inadi na Ustadh Karim Swahibu la kua majaji katika shindano hili muhimu, picha zilizo shiriki kwenye maonyesho takriban zilikua (300) za wapiga picha (300), kazi ya kuzijaji picha hizo ilipitia awamu tatu, kwana tuliangalia vipengele muhimu katika picha, hapo tukachagua picha arubaini zilizo pata max za juu, kisha tukachakua picha mbili za kwanza, kazi hii tumeifanya kwa muda wa siku kumi (10), mshindi wa kwanza alikua ni bwana Ali Gharabi, na mshindi wa pili ni Abdul-ali Ashtari, na wao wameniomba zawadi zao niikabidhi Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na kupenda kwao kurejesha fadhila kutokana na mwaliko huu mtukufu”.

Akaongeza kua: “Tunatakiwa kufahamu vizuri kuhusu turathi, hazihusu mambo ya kidini peke yake,turathi zipo za aina nyingi sana, kuna turathi za utamaduni, kama vile utamaduni wa Sumar na Baabil pia kuna turathi za kijamii, kama vile turathi za jamii wa waarabu au wakurdi pamoja na jamii zingine, hali kadhalika kuna turathi za mataifa”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa kamati ya majaji wa shindano la hati za kiarabu, pamoja na kutangaza majina ya washindi, ulio wasilishwa na Sayyid Aadil Mussawi rais wa jumuiya ya wataalamu wa hati wa mkoa wa Karbala, alisema kua: “Natanguliza shukrani kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya kongamano hili, ambalo wataalamu wa hati wa Iraq wamepata nafasi ya kushiriki, kamati ya majaji ilikaa na kupitia hati zilizo shiriki katika maonyesho yaliyo enda sambamba na kongamano hili, katika awamu ya kwanza tulichagua kazi 40 za hati na michoro ya kiislamu mbalimbali, bila kusaha kamati ilipitia hati zote kwa kufuata vigezo na masharti yaliyo wekwa katika shindano, na majibu yalikua kama yafuatavyo:

Mshindi wa kwanza ni Farasi Nasrawi kwa hati ya Thuluth anatoka katika (jumuiya ya watalamu wa hati wa kiiraq tawi la Karbala tukufu).

Mshindi wa pili ni Dokta Haazim Abudi Saidi kwa hati za aina mbalimbali, anatoka katika (jumuiya ya watalamu wa hati wa kiiraq tawi la Karbala tukufu).

Hafla ikafungwa kwa kugawa vidani na vyeti vya ushiriki, kwa washindi na kila aliye shiriki katika maonyesho haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: