Bendera za Maimamu wawili wa Askariyyaini zapepea katika milima ya Sanko ya Kashmiri…

Maoni katika picha
Mji wa Sanko uliopo India katika jimbo la Karkal ni moja ya vituo vya ujumbe wa Ataba tukufu za Iraq, Husseiniyya, Askariyya na Abbasiyya zinazo shiriki katika kongamano la Amirul Mu-uminina (a.s), linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, mji huo upo umbali wa kilo meta (50) na unazaidi ya wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) elfu (10).

Wakazi wa mji huo walipo pata taarifa za ujio wa ugeni huo walisimama pande mbili za barabara inayo elekea sehemu watakapo fikia wageni, ambayo ni Husseiniyya ya Muswalaya Mahdi iliyo chini ya taasisi ya Imamu Swaahibu Zamaan (a.f).

Sherehe zilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, iliyo somwa na msomi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Leeth Abedi, kisha ukafuata ujumbe wa wageni kutoka katika Ataba tukufu ulio wasilishwa na Shekh Baasim Karbalai kwa niaba yao. Alianza kwa kuwapongeza kutokana na kuonyesha mapenzi makubwa kwa Maimamu wao (a.s), na mapenzi hayo yanaonekana wazi katika maisha yao, akasema: “Hizi ndio tabia za watu wenye imani na taqwa, na ndio sifa za wafuasi wa Ali bun Abu Twalib (a.s), ambaye kwa utukufu wake na kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake ndio kuliko fanya tukutane na nyie, endeleeni na mwenendo huu utakuokoweni na mtapata radhi za Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na watu wa nyumbani kwake watakatifu (a.s)”. akamalizia kwa kusema kua: “Tunashukuru sana kwa mapokezi mazuri na tunatarajia kua tumetekeleza sehemu ya kongamano letu kwa kufanya sherehe hii”.

Baada yake akazungumza Shekh Naadhir Mahdi mkuu wa hauza ya Ithna Ashariyya, akasema kua: “Hakika ni utukufu mkubwa kwetu kupokea ugeni huu kutoka katika Ataba takatifu za Iraq, ambayo imeendelea kua tukufu kutokana na damu za wanajeshi wake na Hashdi Sha’abi, walio ihami na kufelisha njama za magaidi kutokana na fatwa ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani, tunawashukuru sana wageni wetu kwa kuja katika mji huu na kutupa utukufu kwa ujio wenu”.

Shekh Swadiq Balaghi alizungumza kwa niaba ya taasisi ya Imamu Swaahibu Zamaan (a.f), akasema kua: “Karibuni sana kwa ndugu zenu wapenzi wa Ahlulbait (a.s), karibuni sana enyi ndugu zetu mlio kuja kutoka katika ardhi ya Karbala ya Hussein na Iraq ya Amirul Mu-minina (a.s), mmevumilia tabu za safari na ugumu wa njia hadi mmefika kaskazini ya India mkiwa na manukato ya makaburi matakatifu na harufu ya Ataba tukufu za Iraq”.

Akaongeza kusema kua: “Mmezifurahisha nyoyo za waumini wa mji huu, ambao wanatarajia ipo siku watazuru malalo ya Maimamu (a.s), na wala hawajui kama watapata uwezo wa kutimiza hilo au laa, Mwenyezi Mungu awalipe kwa juhudi zenu tukufu, kwa kitendo hiki mmehuisha utajo wa Muhammad na Aali zake watakatifu, tunawashukuru sana watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa juhudi hizi, sisi wakazi wa mji wa Sanko wanaume kwa wanawake watoto kwa wazee, tunashukuru sana juhudi mlizo fanya na tunashukuru kwa kila hatua mliyo piga”.

Akamaliza kwa kusema: “Fikisheni salamu zetu kwa Maimamu (a.s), baada ya hapo wageni wakaenda kupandisha bendera za malalo ya Maimamu wa Askariyyaini (a.s), na kuzipeperusha katika anga la mji huu mtukufu na kuufanya mlima huu kuo bora kuliko milima yote inayo uzunguka”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: