Imamu Mussa bun Jafari mzuiaji hasira na mdhihirishaji elimu.

Maoni katika picha
Mtawa wa Ahlulbait (a.s) aliye adhibiwa katika jela, mja mwema, nafsi takatifu, pambo la wenye kujitahidi, mtekelezaji mwenye subira, muaminifu mwenye zuhudi, ni mlango wa haja kwa wafuasi wake na wapenzi wake, ni Imamu Mussa bun Jafari Kaadhim, wa saba katika Maimamu waongofu baada ya Mtume, alizaliwa (mwezi 7 Safar 128h), alishuhudia kuanguka kwa utawala wa Umawiyya, utawala ulio eneza uwovu katika ardhi za waislamu, alichukua madaraka rasmi ya uimamu akiwa na miaka thelathini na tano baada ya kufariki baba yake Imamu Swadiq (a.s), Imamu Kaadhim alikua kama baba zake kwa elimu na maarifa, yeye ni katika waendelezaji wa ujumbe halisi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w), aliishi katika zama muhimu sana katika uhai wa waislamu, zama ambazo ilizuka mitazamo mbalimbali ya kimadhehebu na falsafa, jambo lililo fanya kua zama hatari katika historia ya kiislamu, kwani vilidhihiri vikundi vya waovu na vikundi vingi vya kiislamu na ijtihadi mbalimbali.

Bamoja na Imamu Kaadhim (a.s) kubanwa na utawala wa Abbasiyya lakini hakuacha wajibu wake wa kisheria na kidini, wa kupambana na fikra potofu katika uislamu, alifuata mwenendo wa baba zake na babu zake wa kutilia umuhimu mambo ya umma wa kiislamu na kuulinda usipotee, sambamba na kulinda sheria za kiislamu zisipotoshwe, akapambana kwa kutumia elimu aliyo pewa na Mwenyezi Mungu, kwa kufanya mazungumzo na mijadala na watu wenye mitazamo tofauti, hali kadhalika katika zama zake kulikua na uovu wa kuenea kumbi za starehe, alipambana na jambo hilo kwa kulea kizazi cha wanachuoni bora walio beba jukumu la kupambana na kila aina ya uovu ulio taka kuingizwa katika dini ya kiislamu, wakasaidia sana kuzuia upotoshwaji wa dini katika kipindi hicho.

Pamoja na kwamba (a.s) alitekwa na kufungwa na kuhamishwa hamishwa jela moja hadi nyingine, lakini alitumia jela kama fursa yake ya kufanya ibada, upweke wa jela ulimsaidia kufanya itikafu na kujikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, alifunga mcha na kusimama usiku kwa kuswali na kuomba dua, utawala wa Abbasiyya ulitumia kila aina ya vitisha na mateso dhidi yake ya kisaikolojia na kimwili, lakini hawakufanikiwa kumshinda, aidha walitumia kila aina ya mbinu kuficha na kuzuia maneno ya haki aliyo kua akiyasema Imamu kuuambia umma wa kiislamu akiwa jela, lakini hawakufanikiwa, wakajikuta hawana njia ya kumdhibiti (a.s) ispokua ni kumuua kwa kutumia sumu, ndipo wakampa sumu na kumaliza uhai wake tarehe (25 Rajabu 183h) na akazikwa katika mji wa Bagdad pembeni ya soko, kaburi lake leo hii lina minara inayo ng’aa dhahabu, hufurika katika kaburi hilo maelfu ya waislamu kutoka mashariki na magharibi ya dunia wakija kumzuru na kuzunguka kaburi lake, kwa nini isiwe hivyo na yeye ndiye mrithi wa elimu ya mitume na kielelezo cha wacha Mungu, aliye uawa kama walivyo uawa babu zake watakatifu na maadui wa haki wa kibani Umayya na bani Abbasi walio ipenda dunia, hakika aliuawa shahidi akiwa mwenye kufanya subira katika jela za madhalimu.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uawa na siku atakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: