Kiongozi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa ambayo ni sehemu ya kongamano la Rabiu Shahada: Maonyesho haya, yanajenga ukaribu wa mtu na vitabu…

Maoni katika picha
Mkuu wa maonyesho ya kimataifa ya vitabu yanayo fanyika chini ya ratiba ya kongamano la Rabiu Shahada Dokta Mushtaqu Ali amesema kua: “Maonyesho ya vitabu yanajaribu kurudisha ukaribu wa mtu na vitabu, ukizingatia kua ukaribu huo umeanza kupungua katika siku za karibuni kutokana na ongezeko la mitandao ya kijamii”.

Akaongeza kusema kua: “Kwa hiyo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wamejitahidi kuhakikisha maonyesho haya yanafanyika na kutoa huduma kwa watu, na kuhakikisha jambo hili linakua endelevu katika tukio hili na mengine kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Akabainisha kua: “Kamati ya maonyesho imezingatia kua na vitabu vya maudhui mbalimbali zinazo lenga watu wa tabaka zote katika jamii, watoto, wazee, familia, wanaume, wanawake, watu wa sekula, watu wa dini hadi mazuwaru”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika maonyesho haya ni sehemu ya kongamano la Rabiu Shahada, safari hii zimeshiriki nchi saba, ambazo ni: (Lebanon, Iran, Sirya, Misri, Ungereza pamoja na nchi mwenyezi wa maonyesho haya Iraq) huku kukiwa na vituo na taasisi za usambazaji zaidi ya (133) kutoka katika nchi hizo”.

Kumbuka kua maonyesho haya yalianza siku ya Juma Pili (28 Rajabu 1439h) sawa na (15 Aprili 2018m) katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu lililo pauliwa, na yataendelea kwa muda wa siku (10), kuanzia siku ya (28 Rajabu 1439h, sawa na 15/4/2018m) hadi (8 Shabani 1439h, sawa na 25/4/2018m), jumla ya ukubwa wa eneo la maonyesho ni zaidi ya (2m3000).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: