Akaendelea kusema: “Katika siku chache ambazo nimekua hapa nimefanya ziara mara nyingi katika malalo mawili matatukufu, kila mara nilikua napata hisia tofauti, nilipata hisia tofauti kwa Abulfadhil Abbasi hali kadhalika naendelea kupata hisia tofauti, bado malalo hii inaendelea kutoa hisia kutokana na kufungamana kwake na Imamu Hussein (a.s), navutiwa na sifa za pekee za Abulfadhil Abbasi (a.s), alikua na upekee maalumu unaweza kuhisi hilo utakapo kua ndani ya malalo yake tukufu, hakika alikua ni kielelezo cha utiifu na kweli yeye ni mlango wa haja (baabu hawaaiji)”.
Akasisitiza kua: “Katika zama hizi za utandawazi, iwapo ulimwengu ukitafuta uislamu halisi, atachomoza Imamu Hussein (a.s) kama nuru na njia inayo faa kufatwa na watu wa imani zote, hakika heshima yake, vitendo vyake na mafundisho yake yanafika mbali zaidi ya dini, imani, utaifa, rangi na utamaduni, hakika yeye ni mwakilishi wa binadamu wote, msimamo wake ulikua dhidi ya utwaghuti na vitendo vibaya, vitendo vyake vinawakilisha mafundisho ya mitume na mawasii wote:
- 1- Hakika yeye ni ngao ya watu wote wanao upenda uislamu katika dunia nzima.
- 2- Hakika yeye ni msuluhishaji wa watu wote duniani.
- 3- Hakika yeye ni mfano wa kweli katika kujitolea na kufanikisha islahi.
Watu waamke, watoke katika kughafirika kila mmoja atayaona haya.