Sayyid Swafi akutana na wageni wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada na awahakikishia kua Iraq ipo salama na imepata amani kwa utukufu wa raia wake na kuitikia kwao fatwa ya Marjaa dini mkuu…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi amesisitiza kua Iraq ipo salama na imepata amani baada ya kulengwa kwa mashambulizi, tumeweza kushinda njama zote dhidi yetu, zilizo kusudia kuharibu utamaduni wetu na mustaqbali wetu, ushindi huu umepatikana kutokana na kujitolea kwa raia wa Iraq na kuitikia kwao fatwa tukufu ya kujilinda, iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu.

Haya aliyasema alipo kutana na idadi kubwa ya wageni wa kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada katika mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika Iraq imefanya kazi kubwa sana katika kulinda umoja wa taifa lake ardhi yake na maeneo matukufu, imetoa maelfu ya mashahidi miongoni mwa wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi, na makumi ya maelfu majeruhi, alhamdu lilahi, tumeshinda njama zote zilizo pangwa na maadui dhidi ya taifa hili, njama za magaidi madaesh hazikufanikiwa, Iraq imeibuka mshindi dhidi ya hatari iliyo kua inaikabili sio kwa wairaq peke yao bali ilikua ni hatari kwa nchi zote za kieneo, hakika raia wa Iraq wapo imara pamoja na hatari zote zinazo wazunguka, karibuni sana katika nchi yenu ya pili Iraq, ambayo tunatarajia siku za mbele iwe bara zaidi, na tunatamani kukutana tena na nyie”.

Tunapenda kukumbusha hapa kua, Sayyid Swafi amesha wahi kusema kua: “Kuna vitu viwili vikuu vilivyo saidia kupatikana kwa ushindi wa Iraq, kitu cha kwanza: ni fatwa tukufu, ambayo inawakilisha mwendelezo wa historia ya mji wa Najafu Ashrafu, na kitu cha pili: ni mwitikio wa haraka wa fatwa ya kujilinda, vitu hivyo ndio vilivyo leta ushindi mkubwa ulio patikana ndani ya muda mfupi.

Leo hii tuna idadi kubwa ya mashahidi, lazima jambo hili litaendelea kua historia, tuna zaidi ya mashahidi laki nane –nazungumza mashahidi wa Hashdi Sha’abi- na zaidi ya majeruhi (22000), watu hawa walijitolea kila walicho nacho huku roho zao zikiwa na utulivu, wakiamini kua wanafanya jambo linalo kubaliwa na sheria na lina fatwa tukufu, kuna baadhi wamepoteza viungo vyoa lakini utawakuta ni wenye kutabasamu na kufurahi, wanasema: fatwa hii imetuletea rehma, tulikua tunaisubiri kwa hamu. Pamoja na kwamba wamepoteza viungo vyao lakini hawajutii nafsi zao, hii inaonyesha msimamo walio nao katika nafsi zao na hata katika nafsi za watu wengine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: