Kikao kiliongozwa na Dokta Swabiih Ka’abi, kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu zikawasilishwa tafiti zifuatazo:
- 1- Shekh Muhammad Jawaad Lankarani kutoka katika mji wa Qum nchini Iran, utafiti wake ulikua unasema: (Harakati za Husseiniyya na mazingira halisi ya uislamu).
- 2- Shekh Nizaar Muhammad Shauki kutoka Qatif nchini Saudia, utafiti wake ulikua unasema: (Athari ya misimamo ya kiimani katika kumjenga mpiganaji (mujahidin).. Bariri bun Khadhiir (r.a) kama mfano).
- 3- Shekh Abbasi Ali Kaashifu-Ghitwaa kutoka Iraq, utafiti wake ulikua unasema: (Mradi wa fatwa tukufu ya kujilinda).
Tafiti hizo zimeibua mambo ambayo hayakuwahi kuzungumzwa sana siku za nyuma, na zimepata mwitikio mkubwa, ikiwa ni pamoja na michango mbalimbali kutoka kwa wahudhuriaji, na mwisho watafiti wakapewa zawadi.