Wageni na viongozi wa madhehebu na dini tofauti wamekutanishwa na mapenzi ya Imamu Hussein (a.s) katika mji wake na kufahamiana…

Maoni katika picha
Mwandishi wa kimasihi bwana Antoni Bara anasema: “Hakika Hussein (a.s) ni kiungo muhimu katika dini, kama sio yeye dini za Mungu zisinge fundishika, uislamu ulianzishwa na Muhammad na ukaendelezwa na Hussein, na Zainabu (a.s) alimalizia kazi ya jihadi na kuilinda dini”.

Miongoni mwa ratiba za siku ya kwanza ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu shahada awamu ya kumi na nne, linalo simamiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya mwaka huu chini ya kauli mbiu isemayo: (Tumepigana kwa utukufu wa Imamu Hussein (a.s) na tumeshinda kwa utukufu wa fatwa), jioni ya jana Ijumaa (3 Shabani 1439h) sawa na (20 Aprili 2018m) kimefanyika kikao cha kutambuana kwa wageni wanao shiriki katika kongamano ambao wanatoka katika nchi tofauti na jamii tofauti katika moja za kumbi zilizopo katika mji wa Imamu Hussein (a.s) wa mazuwaru ambao upo chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu.

Pamoja na kutofautiana kijografia na kijamii kwa wageni wetu lakini wanaunganishwa na mapenzi yao kwa Imamu Hussein (a.s), kongamano hili ni fursa ya kutambuana baina yao, kwa ajili ya zowezi la kutambuana, kamati ya maandalizi ilitenga muda maalumu wa kufanya kikao cha kutamulishana baina yao.

Kikao hicho kilifunguliwa na ujumbe kutoka kwa wageni washiriki, ulio wasilishwa na muasisi wa umoja wa waislamu nchini Marekani Sayyid Hassan Qazwini, ambaye alisema kua: “Hakika kuwepo kwetu katika ardhi ya Karbala mji wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kongamano la Rabiu shahada ni moja ya ukweli wa aya isemayo: (Hakika tumekuumbeni mwanaume na mwanamke na tukakujalieni mataifa na makabila ili mpate kutambuana, hakika mbora wenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni mcha Mungu wenu)”.

Ukafuata ujumbe wa Ustadh Muyassir Hakim mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano, akaelezea kwa ufupi kuhusu miradi inayo fanywa na Ataba mbili tukufu, akabainisha kua: “Ataba mbili tukufu zinafanya kila ziwezalo kwa ajili ya kuboresha huduma kwa mazuwaru wa mji wa Karbala kwa ujumla, huduma hizo zimegawanyika katika miradi ya kiujenzi na kihuduma pamoja na miradi ya kitamaduni inayo toa huduma za kielimu na kimaadili, miongoni mwa miradi inayo toa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru ni ujenzi wa majeno ya mazuwaru katika barabara kuu zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala, na sisi hivi sasa tupo katika moja ya majengo ambayo yamejengwa rasmi kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru, ambayo yanaitwa mji wa Imamu Hussein (a.s) wa mazuwaru”.

Kikao hicho kilipambwa na kuangalia filamu iliyo onyesha namna wairaq walivyo itikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda, na namna walivyo ingia vitani kulinda ardhi yao na maeneo matakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: