Usiku wa kukumbuka kuzaliwa kwa mtu anaye fanana zaidi na Mtume (s.a.w.w)…

Maoni katika picha
Katika usiku kama huu mwezi kumi na moja Shabani, ni usiku wa kukumbuka kuzaliwa kwa mtu anaye fanana zaidi na Mtume (s.a.w.w) kimaumbile na tabia, ambaye ni Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), na jina lake la kuniyya anaitwa Abulhassan, mama yake ni Laila mtoto wa Abu Urwa bun Masuod Thaqafiy, Urawa alikua miongoni mwa watu wanne watukufu katika uislamu, na miongoni mwa watu mashuhuri.

Aliuawa shahidi bamoja na baba yake Hussein (a.s) katika ardhi ya Karbala, na akazikwa karibu na kaburi la baba yake, waislamu huwenda kwa wingi kutembelea kaburi lake tukufu.

Wana historia wametofautiana kuhusu umri wake, kuna wanao sema alikufa akiwa na miaka kumi na nane, na Shekh Mufid katika kitabu chake cha Irshaad amesema: alikufa akiwa na miaka (19), na wemgine wanasema alikua na miaka (25), pia wametofautiana kuhusu yeye ndiye mkubwa kwa umri au Imamu Sajjaad (a.s), inasemekana yeye ndiye mkubwa kama alivyo sema Shirazi Thani na jopo la wanachuoni, bali hilo ndio mashuhuri zaidi.

Ali Akbar (a.s) alikua sawa na baba zake watukufu, alijulikana kwa ukarimu wa wageni, kuwapa chakila masikini na kumkarimu kila anaye mtembelea, alikua na kiwango cha juu cha tabia njema na ukarimu, kwa nini asiwe hivyo, wakati amezaliwa katika nyumba yenye kiwango cha juu cha imani na taqwa, nyumba ya watu ambao wamesimama imara kulinda misingi halisi ya uislamu, na wameshikamana nao vilivyo, na ndio wanyanyuaji wa bendera ya aqida, bali nyumba hiyo ndio kielelezo cha aqida, nyumba ambayo kila mwenye imani ya dini anatakiwa aipende na kuihami, na ajitenge na kila mwenye kuipiga vita.

Amekulia katika mazingira ambayo anakula maziwa ya waumini na wacha Mungu, mwili wake ukakuzwa na virutubisho salama na roho takasifu, alikula na kunywa vitu halali visivyo changanyika na batili wala vitu vyenye utata.. alikua katika mazingira bora zaidi ya ucha Mungu, muda ukaisha siku zikapita, akapata sifa za pekee katika uhai wake zilizo bakia karne na karne, alikua ni kijana mwenye tabia nzuri katika maisha yake yote, pia ni mtu jasiri na shujaa mkubwa.

Inasemekana alikua anafanana zaidi na babu yake Mtume (s.a.w.w), habari hii haikupokewela na wapokezi wa hadithi au wana historia, ni habari iliyo simuliwa na watu walio muona Mtume na wakamuona yeye bayana, alithibitisha jambo hili baba yake mzazi Imamu Hussein (a.s), watu wamepokea kutoka kwake na wana historia wameandika kutoka kwake moja kwa moja, ukizingatia kua Imamu Hussein (a.s) alikua anamjua zaidi Mtume kushinda watu wengine, na alikua mtu wake wa karibu zaidi, alipo mzaa mwanaye Ali Akbar, akawa anawaambia watu kua mtoto huyu anafanana sana na Mtume (s.a.w.w) kuanzia sura, tabia na mwenendo wake kwa ujumla, hadi ilifikia watu wa Madina wakiwa na hamu ya kumuona Mtume (s.a.w.w) wanakwenda kumuangalia yeye, hakika hakuna mtu mwingine zaidi ya Imamu Hussein (a.s) aliye kua akiwajua zaidi watu hawa na utukufu wao.. ni lazima tuamini maneno yake yanayo thibitisha kua mwanaye anafanana sana na Mtume kimaumbile, kitabia na mwenendo mzima, kwani hakika yeye ni muaminifu na mkweli zaidi.

Ali Akbar alikua na uso mzuri sana na tabia nzuri zaidi kwa mujibu wa makubaliano ya wana historia, pia wamekubaliana na maneno ya baba yake kua, alikua anafanana zaidi na Mtume kimaumbile, tabia na uongeaji.

Amani iwe juu yake siku aliyo zaliwa na siku aliyo uawa shahidi na siku atakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: