Kituo cha Alkafeel cha utamaduni na habari za kimataifa chatoa aprication yake mpya (Uismamu... kwa nini?).

Maoni katika picha
Kituo cha Alkafeel cha utamaduni na habari za kimataifa, kutokana na harakati za idara ya habari za kwenye mitandao, kimetoa aprication (App) mpya itakayo ingizwa katika mtandao rasmi kwa jina la (Uislamu... kwa nini?), aprication hiyo inavitu mbalimbali vinavyo fanana na vile vilivyomo katika toghuti, tofauti yake ni kwamba vitu vilivyomo katika aprication hii vinaendana na matumizi ya simu ganja.

Mkuu wa kituo cha Alkafeel cha utamaduni na habari za kimataifa ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jasaam Mahammad Saidi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Aprication (App) inahusika na kujibu maswali muhimu, kwa mfano: kwa nini tunahitaji dini? Na kwa nini iwe ni dini ya kiislamu? Mtume Muhammad ni nani? Tutajibu zaidi shubha zinazo tolewa na wasio kua waislamu, kama vile, ni kipi kitabu kitukufu cha waislamu? Pamoja na kujibu shubha kuhusu kitabu hicho pia, sambamba na maswali kama vile, ni ipi itikadi ya kiislamu? Uislamu umeweka utaratibu gani wa maisha? Utajibu vipi shubha kama uislamu hauendani na maisha.

Akaongeza kusema kua: “kuna milango ya habari, makala na picha za video, pia kuta tv ya kwenye mtandao wa You Tube na tumesha ingiza zaidi ya video (32) na bado tunaendelea kuandaa vipindi vingine vingi kwa ajili ya tv hiyo, vitakamilika hivi karibuni Inshallah na kuingizwa kwa jina hilo hilo (uislamu...kwa nini), tv hiyo itakua na vipindi vya utamaduni, dini na elimu. Tunapenda kufahamisha kua (uslamu ...kwa nini? Ni aprication inayo walenga wasio kua waislamu, lakini pia inawalenga waislamu wanao penda kujifunza mambo mapya na kutaka kujua falsafa ya dini kwa ujumla.

Akafafanua kua: “Hii ni aprication ya aina yake katika ulimwengu wa kishia, pia ni ya aina yake katika Ataba tukufu, imetengenezwa na watalamu wa Maahadi ya Alkafeel ya kutoa elimu na kukuza vipaji, na kupangiliwa vizuri na kuwekewa ulinzi imara, unaweza kuipata katika (Google Play) na hivi sasa inapatikana katika (iOS ) na baada ya siku chache itaingizwa katika App Store.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: