Kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya chatoa maelekezo maalumu kuhusu ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani na chasisitiza yazingatiwe…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu za Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetoa maelekezo kwa viongozi wa mawakibu na vikundi vya kutoa huduma vitakavyo shiriki katika kuhudumia mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani, na kimesisitiza kuheshimiwa kwa maelekezo hayo kwa ajili ya kuhakikisha ziara inafanyika kwa amani na usalama, jambo ambalo linalinda heshima ya ziara hii na utukufu wa eneo hili, na kuhakikisha kua halifanyiki jambo litakalo haribu sura ya ziara hii tukufu.

Maelekezo yaliyo tolewa ni:

  • 1- Kulinda utukufu wa mji wa Karbala kwa kuswali kwa wakati sehemu hiyo hiyo ilipo maukibu na kama ikiwezekana waswali jamaa.
  • 2- Kuheshimu na kufuata maelekezo yote yanayo tolewa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
  • 3- Kazi zifanyike ndani ya eneo walilo pangiwa bila kutoka nje ya mipaka.
  • 4- Kuondoa aina zote za uchafu utakao zalishwa na maukibu au kikundi katika kazi zao.
  • 5- Watumishi wa maukibu au kikundi wazingatie kanuni na maelekezo yanayo tolewa na Ataba mbili tukufu, tunasisitiza kutofanya jambo lolote ambalo lipo kinyume na maadili au linapingana na sheria tukufu.
  • 6- Kuweka bango la utambulisho linalo onyesha jina la maukibu au kikundi na jina la kiongozi wake pamoja na namba ya kitambulisho kilicho tolewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu.
  • 7- Kazi za maukibu au kikundi zisiathiri shughuli za wafanya biashara, mahoteli, watembeaji na upitaji wa magari yanayo toa huduma, wala zisiathiri utulivu wa mazuwaru na vituo vya ukaguzi.
  • 8- Wazingatie kuondoa hema zao na kila kitu walicho weka baada ya kumalizika ziara ya Shaabaniyya.
  • 9- Inaruhusiwa kutumia gesi tu, katika kupika.
  • 10- Hairuhusiwi kuinua alama za kidini au kisiasa katika maukibu, ili ushiriki wako uonekane ni kwa ajili ya Ahlulbait (a.s) peke yao.
  • 11- Vipaza sauti visiwashwe kwa sauti ya juu na vizimwe wakati wa adhana na swala.
  • 12- Hairuhusiwi kufyatua fataki na aina zote za michezo ya aina hiyo ambazo hufanywa mara nyingi katika sherehe za harusi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: