Zaidi wa maukibu za kutoa huduma (600) zinashiriki kuwahudumia mazuwaru katika usiku na mchana wa nusu ya mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya za Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza kua mawakibu zinazo shiriki kutoa huduma katika ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ni (654) ndani na nje ya mkoa wa Karbala, chini ya mipaka yake ya kiutawala na wale walio jisajili rasmi katika kitengo hicho.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Na’mat Salmaan, ambaye alisema kua: “Maukibu hizo zimeenea katika njia zote zinazo ingia ndani ya mji mtukufu wa Karbala, kutokea upande wa Huru, upande wa Najafu, upande wa Baabil, upande wa Bagdad, pamoja na mawakibu nyingi nilizo enea ndani ya mji wa Karbala, na kuna maukibu moja ni ya watu wa Pakistani”.

Akabainisha kua: “Hakika maukibu hufanya kazi ya kutoa huduma za chakula, malazi, vinywaji na tiba, huduma hizo hutofautiana katika kila maukibu, maukibu zimepangwa kutokana na utaratibu ulio wekwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, ambapo kimeainisha sehemu ya kukaa maukibu, jina la kiongozi wa maukibu pamoja na kitambulisho kutoka katika idara ya usalama ya mkoa”.

Bwana Salmaan akabainisha kua: “Kwa ajili ya kuhakikisha tunapata mafanikio mazuri yanayo endana na utukufu wa ziara hii, na kuhakikisha tunaondoa kila aina ya vikwazo katika utekelezaji wa ziara, tulifanya vikao mbalimbali vya kutoa maelekezo kwa viongozi wa mawakibu na wakatoa ahadi za maandishi kua wataheshimu na kufuata maelekezo na kanuni walizo pewa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: