Msafara wa muache akiwa mzuri zaidi (Khaluha Ajmal) ulianzia katika mkoa wa Mosul, baada ya kukombolewa kwa mji huo kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh, kikundi cha watu hao kilianza kusafisha barabara za mji huo na kuondoa athari za mabaki ya vita, nacho ni kikundi huru cha watu wanao jitolea, kilicho kusanya vijana wa mji wa Mosul wenye mitazamo na dini tofauti wanao onganishwa na kitu kimoja kikuu ambacho ni Iraq, lengo kuu ni kujitenga na ubaguzi ulio letwa na kundi la kigaidi na kuhubiriwa kwa miaka mitatu.
Baada ya msafara wa (Alwafaa) ulio fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kusimamiwa na kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji walio fanya usafi katika mji wa Mosul, ndipo ikaja fikra ya vijana hawa nao kuja katika mji mtukufu wa Karbala na kufanya kitu ambacho kitaonyesha japo kidogo kulipa fadhila kwa kile kilicho fanywa na Ataba tukufu katika mji wao, ikiwa ni usafi au ukombozi wa mji wao.
Pia Atabatu Abbasiyya tukufu imewasaidia katika baadhi ya mambo, kama vile kuwapa usafiri wa kuwaleta katika mkoa wa Karbala na kuwapa nyumba ya kulala inayo wafaa katika mji huu, shughuli zao zilianza katika ziara ya mwezi kumi na tano Shabani na zinaendelea baada ya ziara, wanafanya kazi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kugawa chakula na maji kwa Mazuwaru, na baada ya ziara wameanza kusafisha baadhi ya barabara za mji wa Karbala.
Bwana Omari Saarati mmoja wa washiriki wa msafara huu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Msafara wa muache akiwa mzuri zaidi (Khaluha Ajmal) ni msafara wa vijana wa Mosul wanao jitolea kufanya usafi na kutoa misaada kwa wakimbizi wa Mosul baada ya kuondoka kwa wingu la magaidi wa Daesh, na baada ya kuwepo kwa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji katika mji wetu na kuunda kwao msafara wa (Alwafaa) ulio fadhiliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ndipo tulipo anza kuwasiliana nao kwa ajili ya kuja Karbala, baada ya kupata washiriki (85) wa kujitolea tumekuja Karbala, na safari yetu imesadifiana na ziara tukufu ya mwezi wa Shabani, tumeandaa chakula na vitafunwa vya kimosul na kugawa kwa mazuwaru, pia tumetengeneza ukuta mkubwa ambao tumechora picha ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) na minara mitukufu, na katikati yake kuna mikono miwili ikiwa kama ishara ya umoja wa raia wa Iraq wa mitazamo na tabaka tofauti”.
Akamaliza kwa kusema: “Lengo kuu la msafara huu kuja hapa katika mji wa Imamu Hussein (a.s) ni kutuma ujumbe wa amani na mapenzi na kuwajulisha walimwengu kua; wananchi wa Iraq ni wamoja hawata tenganishwa na vyama wala ukabila, njama waliyo jaribu kuipandikiza maadui na wameshindwa, hali kadhalika ni sehemu ya kulipa fadhila kwa watu wa Karbala na watu wa mikoa ya kusini walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kuukomboa mji wa Mosul na mikoa mingine ya Iraq iliyo kua imevamiwa na magaidi ya Daesh, tunatarajia kufanya msafara mwingine katika ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) tukiwa na idadi kubwa ya watu wanao jitolea Inshallah.