Kupitia ukurasa wa ziara kwa niaba: Mtandao wa Alkafeel umefanya ziara zaidi ya (11000) za nusu ya mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Kupitia ukurasa wa ziara kwa niaba na baada ya kufanya baadhi ya marekebisho ya kiufundi, Mtandao wa kimataifa Alkafeel –ambao ni mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu- umefanya ziara kwa niaba na kusoma dua maalumu ya ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani kwa watu walio jisajili katika mitandao yake yote ya (Kiarabu, Kiengereza, Kifarsi, Kituruki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswahili na Kijerumani), watu wote walio jiandikisha katika ukurasa huu walifika (11,140) kutoka katika nchi tofauti za kiarabu na kiajemi.

Ibada ya ziara kwa niaba ya nusu ya mwezi wa Shabani ilihusisha, ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na swala ya rakaa mbili na dua maalumu, hakika ukurasa wa ziara kwa niaba upo tayali kumfanyia ziara kila mtu atakaye jiandikisha katika ukurasa huu, kupitia lugha yeyote katika lugha zilizope kwenye mtandao wetu, au unaweza kuingia kupitia anuani hii: https://alkafeel.net/zyara/ .

Mtu yeyote atakaye jisajili anaweza kukagua jina lake kupitia anuani hiyo hiyo. Asilimia kubwa ya watu walio jisajili walitoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, India, Saudia, Kanada, Kuwait, Malesia, Australia, Aljeria, Bahrain, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holand, Tunisia, Denmak, Norwey, Qatar, Ubelgiji, Morocco, Afghanistan, Oman, Ekowad, Brazil, Ajentina, Uswis, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Itali, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adhabaijan, Qabrus, Finlend, China, Ailend, Hong Kong, Japani, Imaraat, Sudan).

Idara ya Mtandao wa Alkafeel imeandaa zawadi kwa watu watano miongoni mwa watu walio jisajili kwa ajili ya ziara hii, itafanyika kura kwa ajili ya kuwapata watu hao na majina yao yatatangazwa baadae.

Kumbuka kua ziara kwa niaba ni sehemu za huduma zinayo tolewa na mtandao wa Alkafeel –mtandao rasmi wa Atabatu Abbasiyya tukufu- kwa wafuasi na wapenzi wote wa Ahlulbait (a.s), mtandao huu unamambo mengi ya kielimu na kiutamaduni yanayo msaidia mtu anaye tafuta ukweli.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: