Wazee na watu wenye ulemavu wa viungo wanafanya vipi ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Wakati wa joto kali la kiangazi na baridi kali la kipupwe, utamuona amesimama akiwa na tabasamu akisubiri kupokea wazee na wasio weza kutembea wanao kuja kufanya ziara katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) bila kujali mazingira magumu anayo pitia, akiwa na mkokoteni maalumu (kiti cha mataili) kilicho andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu rasmi kwa kazi hiyo.

Kazi hii inafanywa na idara ya kubeba wenye matatizo maalumu na watu wenye umri mkubwa chini ya kitengo cha utumishi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, huku wakiona kua ni utukufu mkubwa na fahari kwao kuwahudumia mazuwaru, hii ni picha nzuri ambayo inaonyeshwa na watumishi wa malalo hii tukufu.

Idara hii –kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wake Sayyid Riyaadh Khadhir Hassan-: “Idara hii inafanya kazi kwa zamu mbili (asubuhi na jioni) kila zamu wanafanya kazi saa saba, ambapo hubeba watu wenye umri mkubwa na wasio weza kutembea kwa sababu ya maradhi, uzee au ulemavu na kwenda kuwafanyisha ziara”.

Akaongeza kusema kua: “Watumishi wa idara hii wamesambaa kwenye milango mikuu inayo elekea katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanajukumu la kuwabeba mazuwaru wenye mahitaji hayo kwa kutumia viti vya mataili kuanzia sehemu ambayo usafiri wa nje unaishia hadi katika moja ya milango ya haram tukufu, na wakati mwingine humwingiza zaairu hadi ndani ya haram tukufu moja kwa moja hadi katika kaburi tukufu na kumuwezesha kufanya ziara”.

Akamalizia kwa kusema: “Kuna juhudi kubwa za kuendeleza kazi hii na kuhakikisha inafanywa katika mazingira bora zaidi siku za mbele, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya watumishi na viti vya mataili vya kisasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: