Atabatu Abbasiyya yakamilisha maandalizi ya kuupokea mwezi wa Ramadhani na yaandaa ratiba maalumu…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, na imeandaa ratiba maalumu ya usalama na utumishi kwa mazuwaru wanaokuja kwa Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Ratiba hiyo inalenga kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wanaokuja katika eneo hili tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku hizi tukufu na kufanya ziara pamoja na kusoma dua kwa urahisi na utulivu.

Ratiba ya Ramadhani inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: Kisomo cha Qur’an tukufu ambacho watashiriki wasomi wa kimataifa kila siku alasiri (jioni) watasoma juzu kamili.

Pili: Kisomo sha Qur’an kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na mazuwaru baada ya swala ya Dhuhurain ndani ya ukumbi wa haram tukufu.

Tatu: Kisomo cha Qur’an cha wanawake wa idara ya maelekezo ya kidini ya wanawake watasomea katika moja ya Sardabu (ukumbi wa chini) ya haram tukufu.

Nne: Usomaji wa Qur’an katika kitengo cha Maqamu Imamu Mahdi (a.f).

Tano: Program hizo zitarushwa kupitia masafa maalumu ya matangazo.

Sita: Kisomo cha Dua’aul-Iftitaahi kila siku, au Dua Tawassul siku ya Juma Nne na Dua Kumail usiku wa Ijumaa katika ukumbi wa haram tukufu.

Saba: Utoaji wa mihadhara ya dini kila siku itakayo zungumzia hukumu za funga na maswala ya Ibada.

Nane: Utoaji wa mihadhara kila siku bakla na baada ya swala ya Dhuhurain na kuhitimishwa kwa kujibu ya maswali ya wahudhuriaji.

Tisa: Utoaji wa mihadhara ya dini upande wa wakina mama mazuwaru, katika eneo lao maalumu ndani ya ukumbi mtukufu wa haram utahusisha kujibu ya maswali pia.

Kumi: Kutoa vipeperushi vya kila wiki au kila mwezi kuhusu utukufu wa mwezi huu.

Kumi na moja: Kufanya mashindano ya usomaji wa Qur’an kila siku jioni ndani ya mwezi huu mtukufu.

Kumi na mbili: Kupangilia vipindi maalumu vya kiibada katika kuhuisha siku za Lailatul Qadri.

Kumi na tatu: Kupanga ratiba maalumu kuhusu kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) pamoja na kufanya kongamano la kuzaliwa kwake katika mji wa Hilla.

Kumi na nne: Kufanya ratiba maalumu ya kuomboleza kumbukumbu ya kupigwa panga kwa Imamu Ali (a.s) na kufariki kwake kishahidi.

Kumi na tano: Kuandaa program za mwezi wa Ramadhani zitakazo rushwa katika redio ya Alkafeel ya wasichana.

Kumi na sita: Kuandaa futari na kufuturisha kupitia mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumi na saba: Kuandaa magari ya kubeba mazuwaru katika siku za ziara maalumu au wakati wowote ikitokea tatizo la usafiri kwa mazuwaru watukufu.

Kumi na nane: Kuweka maji ya baridi sehemu zote za ukumbi wa haram na katika maeneo ya karibu na haram kama ilivyo pangwa na idara ya maji katika wakati wote wa futari.

Hivi ni baadhi ya vipengele vitakavyo fanyika katika mwezi huu mtukufu, nafasi haitoshi kutaja vipengele vyote vitakavyo tekelezwa katika mwezi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: