Redio ya Alkafeel ya wanawake wa kiislamu yaandaa vipindi vinavyo endana na utukufu wa mwezi wa Ramadhani...

Maoni katika picha
Redio ya Alkafeel ya wanawake wa kiislamu inayo tokana na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu inaandaa vipindi vinavyo endana na utukufu wa mwezi huu, kwa kiwango kinacho endana na mahitaji ya wasikilizaji wa redio hii wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala, bali hata wasikilizaji wa nje ya Iraq.

Kwa mujibu wa maelezo ya naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu aliyo toa kwa mtandao wa Alkafeel, alisema kua: “Hakika kuna ratiba kamili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu, kuna vipindi vinavyo rushwa moja kwa moja na vipindi vingine vinarekodiwa na kurushwa baadae, vipindi hivyo vinafundisha namna nzuri ya kunufaika na mwezi huu kidini, kiutamaduni na kijamii, kuna mihadhara inayo mlenga mwanamke na familia za kiiraq katika mwezi huu mtukufu, mihadhara hiyo imejaa aya na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s)".

Akaendelea kusema kua: “Ratiba hiyo inahusisha mashindano na mahojiano pamoja na matangazo ya moja kwa moja ya swala ya Ijumaa na kisomo cha Qur’an, ratiba hii itaendelea hadi katika siku za kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na kifo cha Imamu Ali (a.s), ambapo minasaba hiyo imeingizwa katika ratiba”.

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa kwa idhaa ya redio Alkafeel, ni kwa ajili ya kupaza sauti ya raia wa Iraq na mwanamke pamoja na familia za kiislamu, na kujaribu kutatua matatizo ya kifamilia kwa kutumia aya tukufu ambazo hazijaacha kitu chochote ispokua zimetolea ufafanuzi, na kusaidia kutoa malezi sahihi kwa watoto, na imeitwa (Alkafeel) kwa ajili ya kutabaruku na utukufu wa mbeba bendera ya Imamu Hussein Abulfadhil Abbasi (a.s), masafa ya idhaa hii katika Nail Sat ni (MHZ 10727) nyuzi (27500) na frekwens (H) katika masafa ya (FEC3/4), na masafa yake ya Karbala ni (75.3), na katika mji wa Najafu ni (103.9), na Kuut (101.3), na Samawa (91.2), na Basra (101.9), na Diwaniyya (97.3). na Misaan (98.3), na Dhiqaar ni (95.3), na Swalahu Dini –wilaya ya Balad- ni (106.3).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: