Kutokana na kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kufuatia kukamilisha hatua za mwisho katika uwekaji dhahabu kwenye kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) katika awamu ya pili, mafundi na wahandisi wameanza kufanya kazi ya uwekaji wa dhahabu katika ukuta wa nje, kazi hizi zinazo fanyika katika mradi huu zinajumuisha uwekaji wa dhahabu katika eneo linalo julikana kama (Twarima) ambalo linajumuisha eneo la mlango mkuu unao elekea katika haram tukufu inayo tazamana na mlango wa kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s), baada ya kumaliza hatua ya kwanza iliyo husisha sehemu za ubavuni mwa mlango huo upande wa kushoto na kulia.
Rais wa kitengo cha uhandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhayaau Majidi Swaaigh amesema kua: “Tumeanza kufanya kazi za hatua ya pili katika mradi wa kuweka dhahabu sehemu ya mbele ya kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s), awamu hii imeanza baada ya kumaliza ujenzi wa hatua ya kwanza iliyo husisha ukarabati wa ukuta wa zamani, na ikafuatia kazi ya kuondoa vifuniko vya zamani na kuvisafisha na kuvitengeneza upya”.
Akaongeza kusema kua: “Baada ya hapo tulianza kazi ya kukarabati ukuta wote ambayo ilikamilika kwa kutumia njia za kisasa na vifaa vilivyo tengenezwa na shirika la Sika, kwa hatua tano, hatua ya mwisho tulitumia vifaa vya aina ya Kabon ambayo huimarisha zaidi ukuta na kuufanya uishi miaka mingi, pia tukaweka vifaa vya (brc) vinavyo zuia unyevu nyevu kwenye ukuta, ilikuuandaa uweze kubeba vifuniko vya dhahabu”.
Akabainisha kua: “Hakika kazi inaendelea na tayali tumesha maliza uwekaji wa vifuniko vya dhahabu katika mzunguko wa sehemu ya dhahabu, sambamba na kazi hii kuna kazi nyingine inaendelea, ambayo ni kutengeneza vifuniko vya dhahabu vyenye nakshi na maandishi ya herufi za Qur’an, kazi hii inafanywa kwa hatua kutokana na usanifu na ubunifu wa kitengo cha miradi ya kihandisi na kwa kutumia teknolojia ya ngozi”.
Kumbuka kua hatua hii inakamilisha hatua zilizo tangulia za kuweka vifuniko (marumaru) katika nguzo za sehemu ya dhahabu (Twarima) na inaongeza uzuri wa jengo, pamoja na kuhifadhi muonekano wake wa asili tena ukiwa na ufanisi wa hali ya juu, chini ya viwango vikubwa vya ufundi na uhandisi.