Juhudi kubwa za kitablighi zinafanywa na kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya katika mwezi mtukufu wa Ramadhani…

Maoni katika picha
Mwezi wa Ramadhani, ni mwezi mtukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, na ameufanya kua mwezi bora, kila mwislamu anatakiwa autumie vizuri asiache ukapita bila kunufaika nao, kutokana na utukufu wa mwezi huu, kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya kimeandaa ratiba maalumu kwa ajili ya mwezi huu, kwa ajili ya kuchangia kufikia malengo yanayo kusudiwa na kila mwislamu katika mwezi huu, ratiba hiyo inatekelezwa ndani na nje ya Ataba tukufu na hata nje ya Iraq, kupitia makhatibu wanao fanya kazi katika kitengo hiki.

Rais wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu Shekh Swalahu Karbalai ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kutokana na umuhimu wa kunufaika na mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa namna ambayo itaendana na utukufu wa mwezi huu, tumeandaa ratiba ya kitablighi inayo tekelezwa kila siku ndani ya mwezi huu mtukufu, kwa kushiriki watumishi ambao ni Mashekh na Masayyid wanao toa mihadhara na mafundisho ya dini ndani na nje ya Ataba, kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa, inayo jumuisha mada za Fiqhi, Aqida na vitu vingine miongoni mwa hukumu za kisheria, pamoja na maudhui zingine zinazo endana na matukio yaliyopo katika mwezi huu, kama vile kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na kifo cha Kiongozi wa Waumini (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Tunafanya majlisi kila siku katika haram ya bibi Zainabu (a.s) na nyingine katika haram ya bibi Sukaina (a.s), pia tunafanya majlisi katika mikoa ya kusini na katika mji wa Sanjaar, pamoja na majlisi zinazo fanywa kila siku katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu inayo tekelezwa mchana na usiku katika mwezi huu mtukufu, ratiba yenye vipengele vingi vikiwemo vinavyo tekelezwa na kitengo cha dini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: