Pembezoni mwa program zake: Kamati ya maandalizi ya kongamano la kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) yawazawadia wanahabari wa mkoa wa Baabil…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), litakalo anza usiku wa kumi na tano wa mwezi mtukufu wa Ramadhani chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan –a.s- ni muokozi wa waislamu na mfichuaji wa uwovu wa wanafiki) litakalo fanyika kwa muda wa siku tatu, watumishi wa vyombo vya habari vya ndani wamepewa zawadi, pembezoni mwa program za kongamano linalo simamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kusaidiana na uongozi wa wakfu shia wa mkoa wa Baabil na chini ya ulezi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Hafla hiyo imekua na mahudhurio makubwa ya wasomi na watafiti wa Hilla pamoja na wazawadiwa, imefanyika katika bustani za mazaru ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) wa Imamu Ali (a.s) katika makao makuu ya mkoa wa Baabil –mji wa Hilla-, baada ya Qur’an ya ufunguzi kulikua na ujumbe kutoka kwa kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s) Ustadh Najmu Hassanawiy, alitoa shukrani za dhati kwa wanahabari wote kutokana na kazi kubwa wanayo fanya ya kufikisha habari za uhakika kwa walengwa pamoja na kuuelezea mji huu na harakati zake, ikiwemo harakati ya kitamaduni kama hii ambayo tunatarajia kuifanya hivi karibuni, kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) inayo fanyika kwa mwaka wa kumi na moja, na vyombo vya habari vinamchango mkubwa sana katika kutangaza kongamno hili.

Pia kulikua na ujumbe kutoka kwa waandishi wa habari / tawi la Baabil, ulio wasilishwa na rais wao Ustadh Ali Rabiiy, alitoa shukrani za dhati kwa jambo hili kwani linaongeza ushirikiano baina ya jamii na vyombo vya habari.

Katika hafla hii palionyeshwa filamu inayo husu mchango wa vyombo vya habari katika kuelezea ukweli, ikahitimishwa kwa muhadhara wa Dokta Hanaa Jawadi Abdusaadah kutoka katika chuo cha malezi ya elimu za kibinadamu, alizungumzia nafasi ya wanahabari wa Umawiyya katika kupotosha historia ya Ahlulbait (a.s) na kuharibu picha ya Imamu Hassan (a.s) kufuatia utafiti alio uita (Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ni nishati inayo angaza Baqii hadi Hilla).

Mwisho kabisa wanahabari wakapewa zawadi, nao walionyesha kufurahishwa sana kwa kitendo hicho.

Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa makongamano makubwa ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), na linalenga kuonyesha nafasi aliyo kua nayo Imamu (a.s), na kubainisha msimamo wake dhidi ya mtawala wa kipindi chake ambaye ni Muawiya, pamoja na kuangazia mitihani na mateso aliyo pata Imamu (a.s) katika maisha yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: