Wasanii wa kazi za mikono (kuchora) waonyesha ujuzi wao katika kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) na waufanya ushindi wa Iraq kua kauli mbiu yao…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Kwa fatwa yako tumeshinda) kundi la vijana wasanii wa kazi za mikono (wachoraji) ambao wapo katika kikundi cha vijana wa Hamza katika mkoa wa Baabil, wamezindua maonyesho ya picha ambayo hufanywa kila mwaka pembezoni mwa kongamano la kitamaduni la kuadhimisha kuzaliwa kwa Kariim Aalul Bait (a.s) katika awamu ya kumi na moja, linalo simamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan (a.s) chini ya ulezi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Maonyesho hayo yamenafanyika katika mazaru ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) wa Imamu Ali (a.s) katika mji wa Hilla, yamehusisha picha zilizo chorwa katika mbao (mabango), limeshiriki katika maonyesho haya jopo la vijana wanao lelewa na kikundi hicho, kinacho jihusishwa na kuibua pamoja na kuendeleza vipaji vya vijana, wanalea vipaji na kuonyesha maarifa yaliyopo katika akili kwa kupitia michoro ya kwenye mbao, picha za mwaka huu zinaonyesha ushujaa wa wapiganaji wetu watukufu wa jeshi la serikali pamoja na wale wa Hashdi Sha’abi katika kuwang’oa magaidi, pamoja na baadhi ya wapiganaji mashuhuri walio kua na athari kubwa katika vita ya kukomboa ardhi ya Iraq, kama vile Shahidi Abu Tahsiin na wengineo, maonyesho haya yana maudhui za kijamii na mafundisho ya dini.

Watembeleaji wa maonyesho walipewa nafasi ya kushiriki vilevile, walipewa nafasi ya kuchora picha yeyote wanayo ipenda, walijitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo na ikasaidia kuwagundua watu wapya wenye vipaji vya uchoraji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: