Sauti zapazwa kutokana na mapenzi ya Kariim Ahlulbait (a.s) katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwake…

Maoni katika picha
Jioni ya mwezi mtukufu wa Ramadhani katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) Imamu Hassan Almujtaba (a.s), katika Maqaam ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) wa Imamu Ali (a.s), kimefanywa kikao cha usomaji wa mashairi kilicho kamilisha ratiba ya siku ya pili ya kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa Kariim Aalul Bait (a.s) linalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan –a.s- ni muokozi wa waislamu na mfichuaji wa uovu wa wanafiki).

Kisomo cha mashairi kilicho fanywa kwenye mazaru ya Radu Shamsi katika mji wa Hilla, kilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, ikafuatiwa na kisomo cha surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi watukufu, halafu likafuatia neno la ukaribisho lililo wasilishwa na Ustadh Muhammad Hassan Abudi.

Hafla ilipambwa na mashairi mazuri kutoka kwa washairi wa mikoa tofauti ya Iraq, miongoni mwa mikoa hiyo ni: (Bagdad, Waasit, Hilla, Naswiriyya, Samawa na Najafu Ashrafu) waliburudisha masikio ya wahudhuriaji walio kuja kusherehekea kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume mtukufu.

Baada ya hapo zilisomwa shairi na kaswida mfululizo kuhusu kuwapenda Ahlulbait (a.s), na kuwakumbuka walio mwaga damu zao kwa ajili ya taifa hili, pazia ya usomaji wa mashairi lilifunguliwa na mshairi Zainul-Aabidina Saidi kutoka Karbala, akafuata Hussam Hamzawi kutoka Baabil, baada yake akasoma Muhammad Twalib kutoka Karbala, kisha Muhammad Fatwimiy kutoka Baabil, na kuhitimishwa na Muhammad A’ajibi kutoka katika mji wa Ramitha baada ya kaswida iliyo somwa na Raaidu Fatalawi na kukonga nyoyo za wahudhuriaji watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: