Kwa nyoyo zenyu huzuni na machungu: Maukibu ya kuombomleza ambayo hufanyika kila mwaka kwa pamoja baina ya watumishi wa Ataba mbini tukufu katika kumbukumbu ya kifo cha Kiongozi wa Waumini Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s)…

Maoni katika picha
Adhuhuri ya Juma Tano (21 Ramadhani 1439h) sawa na (6 Juni 2018m) imefanyika maukibu (matembezi) ya kuomboleza ambayo hufanyika kila mwaka kwa pamoja baina ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, ikiongozwa na jopo la viongozi pamoja na watumishi wa Ataba mbili tukufu, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mbora wa viumbe baada ya Mtume, Kiongozi wa Waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwani wao ndio wafiwa wakuu.

Maukibu iliyo kua imetanguliwa na jeneza la kuigiza la Kiongozi wa Waumini (a.s), ilianza matembezi yake kwa kutokea ndani ya haram tukufu ya Abbasi, wakapitia katika uwanja wa eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wakati wa matembezi walikua wakiimba kaswida za huzuni zinazo onyesha ukubwa wa msiba huu na namna unavyo umiza nyoyo za waumini na wapenzi wa watu wa nyumba ya Mtume (a.s), walipo fika katika malalo ya Bwana wa Mashahidi Imamu Hussein (a.s) walipokewewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, wakaingia pamoja katika ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) na wakafanya majlisi ya kuomboleza na zikasomwa kaswida za huzuni kutokana na msiba huu mkubwa.

Kwa upande mwingine, Maukibu za watu wa Karbala zilianza kumiminika katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tangu jana jioni, kuja kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya ratiba maalumu iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Mutaqiina na Maula Muwahidiina Ali bun Abu Twalib (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: