Miongoni mwa ratiba za Ramadhani: Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha mihadhara kila siku kuhusu ibada…

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba maalumu za mwezi mtukufu wa Ramadhani, kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha mihadhara ya dini kuhusu ibada, kila siku Alasiri katika ukumbi wa haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na watumishi wa Ataba pamoja na mazuwaru.

Mihadhara inayo tolewa na Shekh Ali Mujaan ni sehemu ya mihadhara inayo simamiwa na kitengo cha dini katika sekta ya tablighi ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na inazungumzia mada muhimu kuhusu ibada, katika kila muhadhara huteuliwa kipengele kimoja katika vipengele vya ibada na kukisherehesha kwa aya na hadithi za Mtume Mtukufu pamoja na hadithi za Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwa ajili ya kuifanya mada ieleweke kwa urahisi sambamba na kutoa mifano hai inayo tokana na mazingira halisi wanayo ishi, hali kadhalika mihadhara hiyo huzungumzia mada za Fiqhi na Aqida.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu, kila mwaka huandaa ratiba maalumu ya mwezi wa Ramadhani, inayo husisha utoaji wa mihadhara ya kifiqhi, kwa ajili ya kufafanua mambo yanayo husiana na hukumu za funga na mengineyo, pamoja na kujibu maswali na kutoa ufafanuzi mbalimbali kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: