Miongoni mwa vutabu viliyo tolewa hivi karibuni baada ya hakikiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ni kitabu cha (Jawaamiul-Jaamii) kilicho andikwa na Aminul-Islam Abu Ali Fadhil bun Hassan Twabarasi (aliye fariki mwaka wa 548h), na kikahakikiwa na Sayyid Jawaad Sayyid Kaadhim Alhakim.
Kitabu kina juzuu sita kimechapishwa na Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji kwa kusaidiana na kushirikiana na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu. Rais wa kitengo hicho Shekh Ammaar Hilali amesema kua: “Hakika kitabu hiki cha tafsiri kipo kati kwa kati baina ya tafsi kubwa ya (Majmaul-Bayani) na tafsiri ndogo ya (Alkafi Alshafi), na alikiandika baada ya vitabu hivyo, akakifanya kua selebasi ya kumfundishia mwanaye Hassan bun Fadhil kama alivyo sema mwanzoni mwa kitabu, alikikamilisha kwa muda wa miezi kumi na mbili, ambayo ni idadi ya makhalifa wa Mtume (s.a.w.w) na viongozi wa umma wa Nabii Mussa (a.s), alianza kukiandika tarehe 18 Safar mwaka wa 542h na akamaliza tarehe 24 Muharam mwaka wa 543h”. Akakisifu kitabu hicho kua: “Ni miongoni mwa tafsiri zilizo bakishwa na zama na kuongezeka thamani yake, tunakitumia katika maisha yetu ya vitendo na kielimu”.
Akaongeza kusema kua: “Hkika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kina furaha kubwa kupata fursa ya kusambaza kutabu hiki katika muonekano mpya, kikiwa kimehakikiwa zaidi na kupangiliwa vizuri faharasi yake kwa namna ambayo inakuwa rahisi sana kwa msomaji kupata sehemu anayo kusudia”.
Rais wa kitengo hicho ametoa shukrani nyingi kwa Sayyid Jawaad Sayyid Kaadhim Sayyid Muhsin Alhakim kwa kuhakiki kitabu hiki, akamtakia mafanikio mema na aendelee kuhakiki vitabu vingine miongoni mwa turathi za kiislamu.