Abulfadhil Abbasi (a.s) na nafasi yake kwa wafuasi wake na wapenzi wake...

Maoni katika picha
Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameinua heshima ya Abulfadhil Abbasi (a.s) duniani na akhera, kwa wapenzi wake na wafuasi wake bali kwa kila mtu, hata Alammah Darbandi katika kitabu chake cha (Asraru Shahada) kama ilivyo katika kitabu cha Maali Sibtwaini, amesifu baadhi ya utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s) alio nao kwa watu.

Kisha angalia katika jina lake tukufu, lipo karibu sana na majina ya Maimamu watakatifu, hauwezi kupita muda ispokua litatajwa na linaheshimiwa zaidi ya majina mengine, hakuna anaye weza kuapa kitu cha uwongo kwa jina lake, kwa sababu ya kuogopa kufikwa na balaa na kufedheheka, hilo limeshuhudiwa wazi.

Kisa cha kutawasali kwake na kukidhiwa haja ni maarufu, haipiti wiki ispokua kuna mtu atapanda mimbari na kusema: Mwenyezi Mungu aitukuze bendera ya Abbasi, na aufanye kua mweupe uso wake, hakika nimekidhiwa haja yangu kwa kumuomba Mwenyezi Mungu kupitia yeye (kutawasali), na kutokana na kufika katika uwanja wake na kuingia katika mlango wake, kisha akasema: Namna ya kuweka nadhiri ni jambo la wazi.

Jambo hili linathibitishwa na mwandishi wa kitabu cha Maali Sibtwaini, pia imeelezewa katika kitabu cha Asraru Shahada Tarikhi Alghaabir wal Muaasir, kila aliye fanikiwa kwenda kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) na akaingia katika raudha yake tukufu ndani ya mji mtukufu wa Karbala, atakidhiwa shida zake, hilo sio jambo la ajabu, Mwenyezi Mungu mtukufu amemtunuku jina la (Mlango wa haja) na akajiwekea kua hatamkatalia mtu yeyote atakaye muomba kupitia mlango huo, yeyote atakaye omba hata nyimwa, bali atawakidhia haja zao na watarudi wakiwa na furaha wenye mafanikio na wakiwa salama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: