Atabatu Abbasiyya tukufu inajiandaa kufanya mambo mawili muhimu, jambo la kwanza ni kumbukumbu ya kila mwaka ya kuadhimisha kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu, kutokana na utukufu wa fatwa hiyo na mwitikio wa wananchi wa Iraq ukapatikana ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, na kuhifadhika ardhi ya Iraq na maeneo matakatifu na kufelisha njama za maadui zilizo lenga kuvunja umoja na mshikamano wa wananchi, kongamano hilo linasimamiwa na kitengo cha habari na uramaduni cha Atabatu Abbasiyya kwa mwaka wa tatu mfululizo, ambalo linaitwa: (Kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda) litaanza Ijumaa (29 Juni 2018m) likiwa na kauli mbiu isemayo: (Ushindi umetokana na nyie ni wenu na nyie ndio washindi), litadumu siku mbili na lina vipengele tofauti, kutakua na mashindano ya picha, visa vifupi pamoja na vikao vya kitafiti na kongamano la jinai ya zama, (mauwaji ya Spaika) sambamba na kutoa zawadi kwa mashahidi na manusura wa mauwaji hayo, pia kutakua na vikao vya usomaji wa Qur’an tukufu na usomamji wa mashairi sambamba na kuzindua kitabu kikubwa kinacho elezea mambo yaliyo fanywa na watu walio itikia wito wa Marjaiyya na wito wa taifa katika matukio ya kivita au ya huduma za kibinadamu au misaada ya kimkakati, pamoja na mambo mengine.
Jambo la pili ni: (Mashindano ya kijana wa Alkafeel ya ubunifu wa kifikra) kwa wahitimu wa vyuo vya Iraq wa udaktari na uhandisi, litakalo fanyika kwa mara ya kwanza katika kiwango hiki tena kwa fani hizi hapa Iraq, ambalo litaanza Juma Tano (27 Juni 2018m) na kudumu siku mbili, mashindano hayo yanakusudia kuchochea vipawa vya kufikiria na kujenga moya wa kushindana baina ya wanafunzi, na kutoa ubunifu wao wa vitu tofauti unao onyesha uwezo walio nao na kuchochea maendeleo ya kielimu, pamoja na kushajihisha wanafunzi wengine kufanya utafiti na kua wabunifu chini ya mwamvuli wa Atabatu Abbasiyya ambaye ndio mlezi wao.
Miradi ya kuhitimu kwa wanafunzi ni matokea ya juhudi zilizo fanywa na mwanafunzi kwa miaka mine au sita, jambo hili tusinge fikia kuona matunda yake kama sio kujitolea kwa watu walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu wa kuilinda Iraq na maeneo matukufu, wakajitolea uhai kwa ajili ya kulinda taifa hili, ambalo maadui wa ubinadamu walitaka kuliharibu na kulivunja na kulifanya kua taifa la wajinga (watu wasio soma), jambo hili tumeliona mara nyingi katika miradi ya wahitimu wa masomo, hawaja sahau fadhila, mara zaote wamekua wakutoa shukrani za dhati na kusifu.