Kwa ushiriki wa waandishi wake: Jarida la Riyadhu Zaharaa lakhitimisha kongamano la waandishi wa habari la tatu…

Maoni katika picha
Chini ya ushiriki wa jopo la waandishi na wahariri wa jarida, kituo cha Swidiqah Twahirah siku ya Juma Mosi ya tarehe (15 Shawwal 1439h) sawa na (30 Juni 2018m) kimekua mwenyeji wa kongamano la tatu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na mwanafunzi bi Hauraa Muhammad kutoka katika Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, ikafuatiwa na ujumbe wa Atabatu Husseiniyya ulio wasilishwa na bibi Khaludu Bayati, ambaye alisema kua: leo imebeba saa tofauti na saa zingine, nayo ni saa ya kuzaliwa kwa jarida la Riyadhu Zaharaa, baada ya kuzaliwa mwanamke mpambanaji, mwalimu, mwenye ubinadamu na mwandishi, watalamu wa jarida la Riyadhu Zaharaa wanafuata nyayo zake kupitia toleo hili la jarida linalo gusa nyanja zote za maisha ya mwanamke ambaye ndio msingi wa kutengeneza familia ya kiislamu na ndiye muhusika pekee anaye mzaa daktari, muhandisi na mwalimu.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mwanamke ndiye anaye unda familia na anapo kua mwandishi wa habari hua na majukumu zaidi, na anapo kua anajitambua huyaelewa majukumu yake” akabainisha kua uandishi wa habari ni jukumu la kumbadilisha mwanamke na jamii kwa ujumla kutoka katika hatua duni hadi katika maendeleo, maneno ni siraha inayo tumiwa na mwanamke dhidi ya maadui zake na maadui wa familia yake, akamaliza ujumbe wake kwa kutoa usia kwa waandishi wa habari wakike, kisha likafuata neno kutoka kwa mwandishi bi Muntaha Muhsin ambaye alielezea uzowefu wake katika ulimwengu wa uwandishi alilo liwasilisha kupitia muhadhara wa maendeleo ya kibinadamu ulio pata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa wahudhuriaji.

Naye muandishi bi Zainabu akashiriki kwa kusoma kaswida kuhusu watumishi wa jarida la Riyadhu Zaharaa na kaswida nyingine kuhusu mji wa Karbala, hafla ikafungwa kwa kugawa vyeti kwa washindi na midani ya kumbukumbu kwa waandishi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: