Kunufaika na likizo za kiangazi na kwa ushiriki wa wanachama (600) wa Skaut: Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel yaanza kutoa mafunzo ya maendeleo kwa ujumla…

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa wanachama (600) wa Skaut na kwa ajili ya kunufaika na likizo za kiangazi na kuzitumia kwa matumizi sahihi, Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutoa mafunzo ya awamu ya pili, yaliyo andaliwa kwa kiwango cha (PDC) ambayo ni ratiba ya mafunzo ya maendeleo kwa ujumla ya tatu kuanzia watoto wanye miaka tisa hadi kumi na nane, kila hatua inafundishwa kulingana na umri wa walengwa.

Ratiba ya elimu, utamaduni, malezi na miongozo ya dini inahusisha ratiba ya vitendo, inavipengele vilivyo wekwa na kusimamiwa na jopo la wabobezi, vinavyo lenga kuwajenga vijana na kuwafanya kua kizazi kinacho jitambua chenye maadili mazuri kilicho pambika na elimu ya kiislamu inayo tokana na turathi za Ahlulbait (a.s), na kusaidia katika kuendeleza vipawa na kuibua vipaji sambamba na kuvitangaza kielimu na kivitendo.

Kufuatia ratiba hii kiongozi wa idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Samad Saalim amesema kua: “Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel inaendesha program ya kielimu na kitamaduni katika viwango vyote kwa ajili ya kupambana na fikra potofu zisizofaa hakika fikra hufutwa na fikra nyingine”.

Akaongeza kusema kua: “Tunahisi tuna jukumu la kufundisha wanafunzi, idara ya watoto na makuzi inafanya kazi kwa bidii ya kufundisha wanachama wa jumuiya ya Skaut ya Alkafeel kwa kufuata ratiba maalumu ya masomo mbalimbali, na kinacho tupa hamasa ni kuungwa mkono na kupewa baraka zote na kiongozi mkuu wa kisheria (Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi) pamoja na rais wa kitengo cha habari na utamaduni kutokana na mambo yaliyomo katika ratiba hii”.

Akabainisha kua: “Leo tumeanza utekelezaji wa ratiba ndefu na iliyo jaa kila kitu, ambayo ilitangazwa na kutambulishwa hapo awali, ratiba hii inatokana na maompi tuliyo pata, na mahitaji ya jamii ya Iraq hasa mji mtukufu wa Karbala katika kipindi cha likizo za kiangazi za mwaka huu, ratiba hizo zitaendeshewa ndani ya jengo la Shekh Kulaini (r.a) lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ratiba ya vipengele vya Skaut imeanza kwa kupandisha bendera ya Iraq pamoja na bendera maalumu ya jumuiya, kisha wanachama wakaelezwa sheria na kanuni zinazo takiwa kufatwa katika Skaut halafu wakala kiapo cha Skaut, kisha washiriki wakasikiliza mawaidha kutoka kwa viongozi, wakasisitizwa kuhakikisha wanafikia malengo ya masomo hayo”.

Kumbuka kua ratiba hii itadumu kwa muda wa miezi miwili na nusu na itahusisha masomo ya aina nyingi, miongoni mwa masomo hayo ni:

  • 1- Masomo ya dini, kama vile Akhlaq, Fiqhi na masomo mengine.
  • 2- Masomo ya kumuandaa kiongozi na kukuza vipaji na kuinua uwezo wa kimwili na kiakili.
  • 3- Masomo ya namna ya kuandaa mahema ya Skaut na kila kinacho jumuisha kujitegemea na kufanya kazi kwa timu.
  • 4- Masomo ya uwandishi wa habari kwa ujumla, na kila kinacho husiana na usanifu, utengenezaji na utoaji.
  • 5- Masomo ya kukuza uwezo wa uwelewa kielimu na kiutamaduni.
  • 6- Kufanya mambo mbalimbali ya kishujaa na mashindano ya michezo kama vile, mpara wa miguu na mingineyo.
  • 7- Kukuza moyo wa umoja na kufanya kazi kama timu moja.
  • 8- Kuongeza maarifa ya wanachama na kuongeza uwezo pamoja na kubaini vipaji vyao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: