Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha ratiba ya mkutano wa Alqamar wa kwanza…

Maoni katika picha
Baada ya siku kumi za mkutano wa Alqamar wa kwanza, ambao ni mkutano wa kitamaduni unaolenga kuenzi utamaduni wa Wairaq, uliosimamiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, na kushiriki zaidi ya watu (100) wa tabaka tofauti, kutoka katika mkoa wa Dhiqaar, wakiwemo watu wa sekula, malezi, na wanafunzi kwa kushirikiana na Mu’tamad Marjaiyya (Mwakilishi wa Marjaa) katika mkoa huo, Alasiri ya Juma Nne (18 Shawwal 1439h) sawa na (03 Juni 2018m) imefanyika hafla ya kufunga mkutano huo katika ukumbi wa chuo kikuu cha Ameed na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya pamoja na katibu mkuu wake.

Baada ya Qur’an ya ufunguzi, ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, miongoni mwa mambo muhimu aliyo ongea ni: “Mji wa Naswiriyya ni miongoni mwa miji mitukufu katika nyoyo zetu na unahistoria kubwa, ni mji wa elimu, maarifa na jihadi, jina lake limefungamana na vita kubwa, sio ajabu mji huu kuandika historia mpya kwa vizazi vijavyo Inshallah.

Kila mtu anatakiwa afikirie daima namna ya kutatua matatizo asiishie kufikiria matatizo pekeyake, kufikiria matatizo peke yake huvunja nguvu na hugeuka yeye kua sehemu ya tatizo, kwa hiyo lazima kila mtu afanye juhudi ya kutatua matatizo anayo yaweza, mtu anapo ona kua matatizo ni makubwa zaodi yake hukata tamaa na hushindwa kutafuta ufumbuzi.

Hakika kukosoa sana humfanya mtu ajishughulishe na mambo yasiyo faa na hurudisha nyuma maendeleo, hususan ukosoaji utakapo kua haulengi kujenga, mtu anatakiwa afanye kazi zaidi ya anavyo sema.

Kwa hiyo ndugu zetu walio kaa siku kumi katika mkutano wa kitamaduni Alqamar wanaweza kupima nafsi zao baada ya hizi siku wanatofauti gani na wamepata faida gani.

Miongoni mwa faida ni:

  • 1- Umekutana na watu uliokua hauwajui, umejifunza kutoka kwao na wao wamejifunza kutoka kwako, umeitambua nafsi yako zaidi kwa kukaa nao.
  • 2- Unaweza kuendeleza elimu kwa kuweka vipawa mbele vyako, jambo litakalo kusaidia kufikia malengo.
  • 3- Kutambua thamani ya muda, mtu anatakiwa kuheshimu muda hakika huisha haraka, na thamani ya kila mtu inatokana na anacho fanya.

Faida hizi bila shaka zitamfanya mtu aone umuhimu wa kujiendeleza na kutatua matatizo ya taifa lake, iwapo atabeba mambo haya katika akili yake na akatafakari namna ya kutatua matatizo, atakua kachangia katika kujenga jamii, bila shaka mkutano huu utatoa watu watakao jali na kuona umuhimu wa kutumia vizuri muda wao kwa kufanya kazi zenye tija na faida.

Mwisho tunawashukuru wasimamizi wa mkutano huu na wote mlio hudhuria, tunamuomba Mwenyezi Mungu ajalie kufikiwa kwa malengo ya mkutano huu”.

Ukafuata ujumbe wa kitengo cha habari na utamaduni ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo hicho Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, alianza kwa kutoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikiwa kwa mkutano huu utakao kua chachu ya kuendelea kufanyika katika mikoa mingine pia, hali kadhalika amewashukuru washiriki wote kwa kuvumilia uchovu wa safari, na akawahimiza kuyafanyia kazi mazuri waliyo yapata katika mkutano huu, akabainisha kua mkutano ulijumuisha masomo, mihadhara, mijadala na mambo yanayo husiana na mazingira halisi wanayo pitia wananchi wa Iraq, kama vile maswala ya kiitikadi, shubuha, upotoshaji wa vyombo vya habari, vita vinavyo zuka kila wakati na namna ya kupambana na changamato hizo.

Washiriki nao walikua na ujumbe ulio wasilishwa na Ustadh Sami Naim, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika ni utukufu ulioje kutoa shukrani zetu za dhati kwa mwakilisi wa Marjaa dini mkuu kwa malezi mazuri tuliyo pata, na kwa Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake”, akabainisha kua: “Hakika ujumbe wa uislamu na ubinadamu ulio fundishwa na dini yetu tukufu unatutaka kutoa ujumbe huu kwa maneno mazuri na fikra tulivu, pamoja na uwezekano wa kuendelea kwa taasisi binafsi na za kijamii kulitumikia taifa hili tukufu”.

Pia kulikua na shukrani zilizo tolewa na mmoja wa washiriki wa mkutano huo Shekh Ali Judah, ambaye aliishukuru sana Atabatu Abbasiyya kwa kuandaa na kusimamia mkutano huu ambao tunatarajia ufanyike tena katika siku zijazo.

Hafla ilipambwa na mashairi pamoja na kaswida, mwisho kabisa washiriki wakapewa vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: