Wataalamu wa Alkafeel wanao toa mafunzo ya uokozi vitani wanaendelea kutoa mafunzo na wahitimisha moja ya mafunzo hayo…

Maoni katika picha
Bado wataalamu wa Alkafeel wanao toa mafunzo ya uokozi vitani wanaendelea kutoa mafunzo kwa mujibu wa ratiba, jana Juma Tano (19 Shawwal 1439m) sawa na (5 Julai 2018m) katika ukumbi mkuu wa jengo la Shekh Kuleini (r.a) wamehitimisha mafunzo ya ishirini na sita yaliyo pewa jina la (Hema la Shekh Karimu Khaqani), ambayo wameshiriki idadi kubwa ya wapiganaji wa Hashdi Sha’abi ambao wamefundishwa kwa nadhariyya na vitende namna ya kutibu watu wanao jeruhiwa katika uwanja wa vita na namna ya kufanya kazi katika mazingira hayo, pamoja na namna ya kuwaondoa majeruhi katika uwanja wa vita na njia za kuwalinda.

Shekh Baasim Karbalai kutoka katika kitengo cha dini wakati anawasilisha ujumbe wa Atabatu Abbasiyya alisema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya na wasimamizi wake wanaendeleza juhudi hii, inayo saidia kuokoa baadhi ya majemedari wanajihadi, mtu anapo soma fani hii atakuja kuokoa mwanadamu mwingine, na mtu anaye sababisha uhai kwa mtu ni sawa na anaye huisha watu wote, muumini lazima avumilie na asubiri, kama ilivyo kua anatakiwa ajiandae kupambana na kila kitu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hivyo anatakiwa ajifundishe vitu mbalimbali na wala asitosheke na kitu kimoja”.

Mkufunzi wa kimataifa bwana Azhar Ali Abdulhussein ambaye ni miongoni mwa wataalamu wa Alkafeel ameongeza kusema kua: “Leo tuna furaha sana kwa kuhitimu kundi hili la watu wanaojitolea, awamu hii inatofautiana na awamu zingine kwa namna ilivyo pangiliwa na wakufunzi, imepangiliwa vizuri sana kielimu kama alivyo sema Shekh Karimu (Jifunzeni ujuzi), na utakapo kua ujuzi huo unahusiana na uhai wa mwanadamu unakua sio kitu cha kudharau, hakika ujuzi huu umefasiriwa katika mazingira halisi ya vitendo, hakika mwongozo wa elimu unao fatwa na wataalamu wa Alkafeel upo chini ya usimamizi wa moja kwa moja na wataalamu wa Ulaya”.

Kamati ya usimamizi wa mafunzo kutoka Ulaya ilikua na ujumbe ulio wasilishwa na mkufunzi wa kimataifa Polandi Sayyid Robati, miongoni mwa mambo muhimu aliyo sema ni: “Kwa mara ya kwanza hapa Iraq na katika nchi za kiarabu watalamu wa Ulaya wanatoa thibitisho la ubora wa kutoa mafunzo ya uokozi vitani kwa watalamu wengine ambao ni wataalamu wa Alkafeel, hakika ni utukufu mkubwa kwangu kuwepo hapa na kusaidia kutoa mafunzo ya utabibu vitani katika mkoa huu, ninawashukuru sana kwa uaminifu wetu kwetu na kwa wakufunzi wetu”.

Wakufunzi washiriki wametoa shukrani zao pia kwa Atabatu Abbasiyya tukufu iliyo wapa fursa ya kupata elimu hii tukufu, wakasema kua: “Shukrani ziwafikie wale walio hangaika usiku na mchana kwa kutufundisha ujuzi wa uokozi vitani ambo husaidia kulinda uhai wa wapiganaji na kuokoa majeruhi”.

Hafla hiyo ilishuhudia maonyesho ya baadhi ya mafunzo waliyo pewa washiriki katika kozi hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: