Miradi ya (Arshu Tilawah) na (Amirul-Qurraau-Watwani) yakutana katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Kuna miradi mingi ya Qur’an tukufu inayo endeshwa na Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa Arshu Tilawah (Arshi ya usomaji) nao ni mradi wa vijana unao lenga kunufaika na vipaji pamoja na uwezo mkubwa wa usomaji wa Qur’an walio nao vijana wa Iraq na kuuonyesha katika ulimwengu wa kiislamu, na kukuza vipaji vyao chini ya utaratibu maalumu, mradi mwingine ni mradi wa Amirul-Qurraau (Kiongozi wa wasomaji), nao ni mradi wa Qur’an ambao unafanywa kwa mwaka wa nne mfululizo chini ya usimamizi wa walimu walio bobea kutoka ndani na nje ya Iraq, unalenga kutengeneza kizazi bora cha wasomi wa Qur’an, kitakacho endeleza Qur’an katika misingi imara, na kuwaandaa vijana wadogo wenye vipaji vya usomaji wa Qur’an kwa kuwaendeleza hadi katika viwango vya juu kabisa katika usomaji.

Miradi miwili hiyo; inasimamiwa na kuendeshwa na kitengo cha kuandaa wasomaji cha Maahadi ya Qur’an tukufu, katika siku tukufu ya Ijumaa miradi hiyo imekutana ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuburudisha masikio pamoja na nyoyo za wasikilizaji na mazuwaru watukufu kwa kusoma Qur’an, wakapendezesha mazingira ya kiroho na pumzi za usomaji wa Qur’an zikawa sambamba na pumzi za Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hafla hiyo ya usomaji wa Qur’an ilifunguliwa na madrasa ya Shekh Abdulfataah Sha’ashai kwa kisomo cha Muhammad Jaasim Swabri kutoka katika madrasa ya Qur’an ya Qal’atu Sukar, kisha akafuata msomaji kutoka katika madrasa ya Shekh Minshawi iliyo somwa na Muhammad Samual kutoka mkoa wa Baadil, halafu ikafuata madrasa ya Shekh Abu Ainain Sha’ishaa ambapo alisoma Ahmadi Jafari Zaruqi kutoka katika Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Baabil, kisha ikafuata madrasa ya Shekh Shahata Muhammad Anwar iliyo somwa na Sajjaad Hussein Rahim kutoka katika taasisi ya Athaqlul-Akbar (Kizito kikubwa) kutoka Bagdad, na mwisho kabisa alisoma mkufunzi Balasim Jaliil kwa mahadhi murua ya kiiraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: